Makahaba hawa wameangaziwa kufuatia kutolewa kwa
kumbukumbu zao na Filamu inayohusu maisha yao. Filamu hiyo, (Meet the
Fokkens), inawaangazia Makahaba mapacha wenye umri wa miaka 70 Louise na
Martine Fokken ambao walitufichulia siri yao katika kufanya ukahaba
katika Mji maarufu zaidi kwa ufuska duniani.
Louise na Martine hutumia muda wao mwingi wakiwa
kwenye Maskani yao ya vyumba viwili katika eneo la Ijmuiden, magharibi
mwa Amsterdam. Huku wakiwa wamevalia viatu vya ndala, wao huranda randa
hapa na pale chumbani wakinywa kahawa na kula keki wakionekana kukosa
muelekeo.
Martine anaimba kwa sauti ya chini
huku Louise akielezea masaibu yaliyoikumba familia yake na kumlazimu
kukimbilia usalama wakati wa Vita vya pili vya Dunia.
Mama yao alikuwa na usuli wa Kiyahudi, jambo
walilofanya kuwa siri kubwa kwa Wanajeshi wa Nazi waliokuwa wanashika
doria nchini Uholanzi. Wimbo wa Louise uligusia Furaha na Huzuni za
maisha.
"Tulikuwa watoto wadogo wakati huo wa vita.
Ving'ora vilipoanza kulia, mama yetu alituficha katika eneo la chini ya
nyumba. hatukuwa na kofia za chuma, hivyo basi tulitumia vikaango vya
kupikia kukinga vichwa vyetu. Tulionekana kuchekesha na kana kwamba
tunafurahia hali hiyo."
Nilimuuliza iwapo maisha wakati huo hapa Amsterdam, yalikuwa ya furaha au kuhuzunisha?
Makahaba mapacha Louise na Martine
Mapacha hao wanasema kutolewa kwa kumbukumbu zao
kumebadilisha muelekeo wao; hapo mbeleni walitusiwa, sasa wanaheshimiwa
"Oh ni kicheko, bila shaka ni kicheko. huna budi kucheka hata unapokuwa
na huzuni kwa sbabu ni maisha yako na huwezi kuyabadilisha, lakini ni
bora ukiwa unatabasamu kila mara."
Dada hao wawili wanatingisa vichwa vya ishara ya kuafikiana katika wanayoeleza.
Hata hivyo, tabasamu lao la kujilazimisha haliepuki kudhihirisha huzuni inayojitokeza machoni mwao.
"Bila shaka hatukuwaza kamwe tulipokuwa na umri
wa miaka 14 au 15 kwamba siku moja tungejiingiza kwenye Ukahaba.
Tulikuwa wabunifu na tulikuwa na Matarajio maishani" akadokeza Martine
says.
Louise naye akaongezea: "kila siku mimi husema
ni mume wangu aliyenipiga na kuniingiza kwenye ukahaba. Alikuwa mtu
anayetumia mabavu na kutishia kutengana nami endapo ningekataa kufanya
ukahaba ili kutafuta pesa.
"Yeye alikuwa kipenzi maishani mwangu…" akasema.
Wanawe Louise' hatimaye wakaishia kulelewa
kwenye makao ya watoto. Alituonyesha mojawapo ya picha zilizopo kwenye
rafu ya vifaa vya kale, inayodhihirisha nyuso zao zenye tabasamu.
Uzoefu wa miaka mingi
Martine bado anafanya Ukahaba. Anasema malipo ay
uzeeni anayopata kutoka kwa Serikali ya Uholanzi hayamtoshelezi
kujikimu kimaishai. Isitoshe anaugua ugonjwa wa Baridi yabisi.
Martine anasema ijapokuwa angependa kustaafu
lakini hawezi kuendelea kujikimu kimaisha. Filamu inayomuhusu
inamuonyesha akiwa kazini, amejipachika kwenye kiti akiwa amevalia soksi
ndefu, mshipi na viatu vya kisigino.
Makahaba mapacha Louise na Martine
Martine Fokken ni kivutio kwa wanaume wakongwe
badala ya vijana wanaompita bila hata kumtazama na kumkejeli kuwa
amezeeka mno. Kama kawaida yake, anaangua kicheko na kusema hajali
kamwe.
Anasema nyakati zimebadilika: "Vijana wa sasa ni
tofauti, wanakunywa pombe sana, wamenona na hawakuheshimu. Wanapaswa
kuwa kwenye pikipiki zao kama wavulana wa Kidachi badala ya kupoteza
wakati wakinywa pombe."
Licha ya ushindani mkali kutoka kwa Vidosho wenye umri mdogo katika eneo la karibu, Martine hakosi wateja.
Anaonekana kuwavutia zaidi Wanaume wazee. Yeye
hutumia vitu wanavyopendelea kuvaa ili kuwavutia kama vile kuingia
kwenye madanguro akiwa na mjeledi huku amevaa viatu vya kisigino kirefu.
Chanzo: BBC