Friday, September 14, 2012
Machafuko yaendelea katika nchi za kiarabu kupinga filamu inayomkashifu Mtume Mohamad
Waandamanaji walioghadhabishwa na
filamu inayodhihaki dini ya kiisilamu wameshambulia balozi za Uingereza na
Ujerumani mjini Khartoum, Sudan.
Waandamanaji walianza kuwasha moto
na kisha kuichanachana bendera ya Ujerumani na kuweka bango lenye maandiko ya kiisilamu
ambapo bendera hiyo ilikuwa.
Taarifa
zinazohusiana
Maandamanao yangali yanaendelea
katika nchi za Mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika kuilaani filamu ya
Marekani inayokejeli Mtume Muhammad.
Mjini Cairo, polisi waliwarushia
gesi ya kutoa machozi na kuwatawanya waandamanaji takriban 500,kutoka katika
ubalozi wa Marekani.
Maandamano pia yalifanyika katika
mji mkuu wa Yemen, Sanaa.
Msemaji wa ubalozi wa Uingereza
amethibitisha BBC kuwa maandamano yanafanyika nje ya ubalozi wa Uingereza na
kusema kuwa polisi wa Sudan wako katika eneo hilo kudhibiti hali.
Hata hivyo, msemaji huyo hangeweza
kuthibitisha ikiwa waandamanaji waliingia katika ubalozi huo au ikiwa
maandanamo yana uhusiano wowote na filamu hiyo inayopingwa na waisilamu kote
dunian
Njama ya mashambulizi yatibuliwa Kenya
Polisi nchini Kenya wamenasa magwanda yenye mabomu ya
kujilipua pamoja na zana zengine ambazo zilikuwa zitumike kwa mashambulizi ya
kigaidi mjini Nairobi.
Washukiwa wawili wamekamatwa katika msako huo uliofanywa asubihi ya leo
katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi.Taarifa zinazohusiana
Msemaji wa polisi nchini Kenya Eric Kiraithe anasema kuwa maguruneti kumi na mbili pamoja na bunduki aina ya AK 47 pia zilinaswa wakati wa msako uliofanywa na polisi mtaani humo."tunaamini kuwa silaha hizi zilinuiwa kutumika kufanya mashambulizi ya kigaidi mjini Nairobi'' alisema bwana Kiraithe.
Msako huo uliofanywa na polisi Ijumaa uliongozwa na polisi wa kupambana na ugaidi baada ya polisi kupata habari kutoka kwa raia.
Na baada ya masaa kadhaa ya kuwahoji washukiwa, magwanda manne ya mabomu ya kujitoa mhanga , mabomu mawili na silaha zingine zilipatikana ndani ya nyumba ya mshukiwa mmoja.
Polisi wanaamini kuwa mabomu hayo yalikuwa na vilipuzi vyenye uzito wa kilo arobaini na yangetumika kushambulia baadhi ya sehemu za mji mkuu Nairobi na miji mingine mikubwa.
Bwana Kiraithe amelaumu kundi la Al Shabab. Amesema kuwa washukiwa wengine 8 wako mbioni baada ya washukiwa Abdul majid Mohammed raia mkenya na Suleiman Abdi Aden msomali, kukamatwa na polisi wa Kenya.
Wangali wanahojiwa na polisi na watafikishwa mahakamani baadaye wiki ijayo.
Silaha hizo zinasemekana kufanana na zile zilizotumika katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika nchini Uganda dhidi ya watu waliokuwa wanatazama fainali ya kombe la dunia mwaka 2010, ambapo watu 76 waliuawa
Kundi la Al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi nchini Uganda, wakisema kuwa wanapinga nchi hiyo kujihusisha na harakati dhidi ya kundi hilo nchini Somalia.
Kenya imeshambuliwa karibuni na kundi la al-Shabab baada ya kupeleka vikosi vyake Somalia.
Rais Kikwete Atembelea Kenya
Rais Kikwete akiangalia kondoo wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho
Rais
Kikwete akiangalia ng'ombe wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda
hicho, n6- Rais Kikwete akiangalia kondoo wanaofugwa kisasa katika
shamba la kiwanda hicho, n7- Rais Kikwete akiangalia mchoro wa ujenzi wa
jengo la kutengeneza maziwa ya unga wa kiwanda hicho. Anayemuelekeza
ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho Kenyatta,
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake baada ya
kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo
Kikuu cha Aga Khan jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara
Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake
ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi
nchini Kenya.
Mkutano wa CHADEMA UINGEREZA
JE, UNAIPENDA TANZANIA?
KAMA JIBU NI NDIYO, BASI NJOO UUNGANE NASI MILTON KEYNES
NJOO UWE SEHEMU YA HISTORIA
NETHERFIELD MEETING PLACE, FARNBOROUGH NETHERFIELD
MK6 4JB kuanzia saa kumi jioni mpaka saa tatu usiku
NJOO UJIUNGE NA MFUKO WA DHARURA
AKINA MAMA NJOONI MJIUNGE NA JUMUIYA YA WANAWAKE CHADEMA
Kutakuwa na usafiri kutoka London na Reading
REFRESHMENTS WILL BE AVAILABLE
kwa taarifa zaidi, tafadhaliwasiliana na wafuatao:-
Mwenyekiti: Mr CHRIS LUKOSI - 07903828119
&
Mwakilishi wa Reading: Mr GERALD LUSINGU
PEOPLE'S POWER!
Souece: Haki Ngowi
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Seif Sharif Hamad, siku ya
Alhamisi tarehe 14/9/12 alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia
maswala ya Afrika Bw. Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao
walibadilishana mawazo kuhusu maswala ya Tanzania na hususan hali ya
kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo hayo yalihudhuria na Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza, Balozi Peter Kallaghe
Makamu
wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akisalimiana na
Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya ya Waingereza walio wahi kuishi
Tanzania (Britain Tanzania Society). Aliyepewa mkono na Mheshimiwa
Makamu wa Rais ni Bwana David Brewin Mhariri wa Jarida la kila mwezi
linalotolewa na BTS, Mama Liz Fennell, Makamu wa Rais BTS (mbele
kulia), Mama Valerie Leach - Katibu (kwanza kushoto), Bwana Dan Coo-
Mwanachama BTS, Bwana Ron Fennel, Afisa wa Miradi ya BTS kwa Tanzania
na Bwana Andrew Coulson, Afisa Mkuu wa Mipango ya Jumuiya hiyo ya BTS.
Makamu
wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akisalimiana na
Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya ya Waingereza walio wahi kuishi
Tanzania (Britain Tanzania Society). Aliyepewa mkono na Mheshimiwa
Makamu wa Rais ni Bwana David Brewin Mhariri wa Jarida la kila mwezi
linalotolewa na BTS, Mama Liz Fennell, Makamu wa Rais BTS (mbele
kulia), Mama Valerie Leach - Katibu (kwanza kushoto), Bwana Dan Coo-
Mwanachama BTS, Bwana Ron Fennel, Afisa wa Miradi ya BTS kwa Tanzania
na Bwana Andrew Coulson, Afisa Mkuu wa Mipango ya Jumuiya hiyo ya BTS.
Makamu
wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akiwa
pamoja na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki. Mheshimiwa Seif
alikutana na Mabalozi hao jana kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania,
London. Katikati ya picha ni Mheshimiwa, Makamu wa Rais, Balozi wa
Tanzania, Mheshimiwa Peter Kallaghe (kushoto), Balozi wa Rwanda,
Mheshimiwa Ernest Rwamucyo (Pili kushoto), Balozi wa Uganda, Mheshimiwa
Joan Rwabyomere (Pili kulia), na Balozi Mdogo wa Burundi, Mheshimiwa
Bernard Ntahiraja (Kwanza kulia).
--
Makamu
wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, aliendelea
na Ziara yake ya jana hapa nchini Uingereza. Mheshimwa Seif, jana
alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia maswala ya Afrika Bw.
Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao walibadilishana mawazo kuhusu
maswala ya Tanzania na hususan hali ya kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo
hayo yalihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,
Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe. Vile vile Mheshimiwa Makamu wa Rais,
aliweza kukutana na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki na Viongozi
wa Jumuiya ya Waingereza waliowahi kuishi Tanzania, ijulikanayo kama
Britain Tanzania Society (BTS).
Leo hii siku ya
Ijumaa, Jioni, kuanzia Saa 18:00pm mpaka saa 21:00, Mheshimiwa Makamu
wa Rais atakutana na Watanzania wote waishio London, katika Ukumbi wa University of London Union, Mtaa wa Malet Street, WC1E 7HY
Watanzania wote wenye nafasi ya kufika mnakaribishwa.
Watakao hudhuria mnaombwa sana kuzingatia muda uliopangwa.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema
Shein,akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za
Wateja,Mussa Ramadhan Haji,kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maji (ZAWA) ikiwa ni miongoni waliochagia katika ujenzi wa Kituo cha
Polisi cha Fumba Mkoa Mjini Magharibi,wakati wa hafla ya ufunguzi wa
kituo hicho jana.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
katika picha ya pamoja na wenyeji wake wa Chuo Kikuu cha Kenyatta baada
ya kufungua Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.Picha na
IKULU
Rais jakaya kikwete akiweka shada la maua kwenye kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya
Rais jakaya kikwete akiweka shada la maua kwenye kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
na Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na
kuweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya,
Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika
Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara
yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi
nchini Kenya.
Thursday, September 13, 2012
ZITTO: TUSISAHAU JAMBO HILI-AZIMIO LILISEMA
Unyonyaji
wa ‘wamjini’ dhidi ya ‘wavijijini’ – Tusisahau jambo hili
Zitto
Kabwe, Mb
Mnamo
tarehe 12 Septemba, 2012 niliandika makala iliyochapwa kwenye magazeti mawili
nchini, Raia Mwema na Tanzania Daima. Makala hiyo ‘Mafukara milioni 30,
Mabilioni 30’ ilikuwa inaonyesha namna ambavyo
mfumo wa uchumi wa nchi yetu ni wa kinyonyaji. Kwamba wakazi wa mijini
wanafaidi zaidi rasilimali za nchi kuliko wakazi wa Vijijini. Vilevile
nilieleza kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania ni wa kifisadi na ufisadi
unafaidisha kikundi kidogo cha watu mijini au wenye tabia za kimjini na hivyo
kukosesha huduma za msingi za wananchi wengi waishio vijijini. Mwanazuoni
kijana Sabatho Nyamsenda ameandika uchambuzi wake mzuri kuhusu makala hiyo kama
‘Tangazo
la Coca Cola na wito wa Zitto dhidi ya Vizito’ ambapo amejaribu kuonyesha kuwa
masikini wa mijini ni sawa tu na mafukara wa vijijini. Sikubaliani naye.
Nitatumia Azimio la Arusha kuboresha hoja yangu na pia mfano halisi wa Mwalimu
wa Kalinzi, Kigoma dhidi ya Mwalimu wa Miburani, Temeke.
Muono
wangu unathibitishwa na mambo matatu. Kwanza ni kuongezeka kwa kasi kwa tofauti
ya kipato kati ya walionacho na wasionacho ambapo sasa kuna kundi dogo la watu
ni matajiri sana na kundi kubwa sana ni mafukara sana. Nilionyesha kuwa
asilimia 30 ya Watanzania wanamiliki asilimia 75 ya Pato la Taifa. Pili,
nilionyesha kuwa kasi ya kupunguza umasikini nchini inaonekana mijini kuliko
vijijini ambapo katika kipindi cha miaka 16, umasikini wa watu wa Dar es
Salaam, kwa mfano, umepungua kwa asilimia 12 wakati umasikini vijijini
umepungua kwa asilimia 2 tu. Tatu, nimeonyesha kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa
vijijini ipo chini ya wastani wa ukuaji wa uchumi wa Taifa kutokana na sekta ya
Kilimo ambayo inaajiri asilimia 75 ya Watanzania imekuwa ikikua ‘flatlining’
kwa asilimia 4 wakati Uchumi wa nchi umekuwa ukikua kwa wastani wa asilimia 7
katika muongo mmoja uliopita.
Nilionyesha
kuwa tabaka la chini la watu wa mijini ni masikini kwani wamepewa fursa za
kuweza kuondokana na umasikini wakati watu wa vijijini ni mafukara kwani mfumo
kwa makusudi umewanyima fursa. Kimombo ninasema watu wa tabaka la chini la
mijini ni ‘poor’ na watu wa vijijini ni ‘impoverished’. Azimio la Arusha
limeonyesha muono kama huu na lilionya kutosahau mwono huu katika andiko lake.
Ninanukuu.
"Vile
vile mkazo wa fedha na wa viwanda unatufanya tukazanie zaidi maendeleo ya
mijini. Tunatambua kuwa hatuwezi kupata fedha za kutosha kuleta maendeleo
katika kila kijiji na ambayo yatamfaa kila mwananchi. Tunajua pia kuwa hatuwezi
kujenga kiwanda katika kila kijiji ili kisaidie kuleta maendeleo ya fedha na
viwanda katika kila kijiji; jambo ambalo tunajua kuwa haliwezekani. Kwa ajili
hiyo, basi, fedha zetu huzitumia zaidi katika miji na viwanda vyetu pia
hujengwa katika miji. Na zaidi ya fedha hizi huwa ni mikopo. Japo zijenge
shule, hospitali, majumba au viwanda ni fedha za mikopo. Hatimaye lazima
zilipwe.
Lakini
ni dhahiri kwamba haziwezi kulipwa kwa fedha zinazotokana na maendeleo ya
mijini au maendeleo ya viwanda. Hazina budi zilipwe kwa fedha tunazopata
kutokana na vitu tunavyouza katika nchi za nje. Kutokana na viwanda vyetu hatuuzi
na kwa muda mrefu sana hatutauza vitu vingi katika nchi za nje. Viwanda vyetu
zaidi ni vya kutusaidia kupata vitu hapa hapa ambavyo mpaka sasa tunaviagiza
kutoka nchi za nje. Itapita miaka mingi kabla ya kuweza kuuza katika nchi za
nje vitu vinavyotokana na viwanda vyetu. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba fedha
tutakazotumia kulipa madeni haya ya mikopo ya fedha kwa maendeleo na viwanda
mijini hazitatoka mijini na wala hazitatokana na viwanda. Zitatoka wapi, basi?
Zitatoka vijijini na zitatokana na KILIMO. Maana ya ukweli huu ni
nini? Ni kwamba wale wanaofaidi maendeleo yanayotokana na fedha
tunazokopa sio kwa kweli watakaozilipa. Fedha zitatumika zaidi katika
miji lakini walipaji watakuwa zaidi ni wakulima.
Jambo
hili linafaa kukumbukwa sana,
maana kuna njia nyingi za kunyonyana. Tusisahau hata kidogo kwamba wakaaji wa
mijini wanaweza wakawa wanyonyaji wa jasho la wakulima wa vijijini. Hospitali
zetu kubwa zote ziko katika miji. Zinafaidia sehemu ndogo sana ya wananchi
wa Tanzania. Lakini kama tumezijenga kwa fedha za mkopo walipaji wa mkopo huo
ni wakulima, yaani wale ambao hawafaidiwi sana na hospitali hizo. Mabarabara
ya lami yako katika miji, kwa faida ya wakaaji wa mijini na hasa wenye
magari. Kama mabarabaraba hayo tumeyajenga kwa fedha za mikopo walipaji ni
wakulima; na fedha zilizonunua magari yenyewe zilitokana na mazao ya wakulima.
Taa za umeme, maji ya mabomba, mahoteli na maendeleo mengine yote ya kisasa
yako zaidi katika miji. Karibu yote yametokana na fedha za mikopo na karibu
yote hayana faida kubwa kwa mkulima, lakini yatalipwa kwa fedha zitakazotokana
na jasho la mkulima.
Tusisahau
jambo hili.
Japo tunapotaja unyonyaji hufikiria mabepari, tusisahau kuwa bahari ina samaki
wengi. Nao hutafunana. Mkubwa humtafuna mdogo na mdogo naye humtafuna mdogo
zaidi. Katika nchi yetu twaweza kugawa wananchi kwa njia mbili. Mabepari na
Makabaila upande mmoja; na wafanyakazi na wakulima upande mwingine. Pia twaweza tukagawa wakaaji wa
mijini upande mmoja na wakulima wa vijijini upande mwingine. Tusipoangalia
tutakuja kugundua kuwa wakaaji wa mijini nao ni wanyonyaji wa wakulima.” Azimio la Arusha,1967. (msisitizo ni wangu).
Azimio
la Arusha limerudia zaidi ya mara moja “Tusisahau jambo hili” ama “Jambo hili
linapaswa kukumbukwa sana”. Tumesahau jambo hili. Licha ya kwamba sisi
wanasiasa wa kisasa tunaona Azimio la Arusha ni nyaraka “outdated” ipo siku tutakumbushwa
kwa njia ambayo hatutakuja kuisahau. Sitaki tufike huko. Mwangwi wa “tusisahau
jambo hili” lazima uendelee kutuonyesha kuwa kuna kazi ya kufanya kuhusu
Mafukara milioni thelathini wanaoishi kwenye vijiji vyetu. Watanzania hawa wa
vijijini hawana fursa za barabara, maji, umeme na hata huduma za jamii kama
wenzao wa mijini.
Nitatoa
mfano mmoja kuonyesha tofauti ya Masikini wa mjini na Fukara wa kijijini.
Wakati nachaguliwa kuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini (jimbo la vijijini) mwaka
2005, ilikuwa inamgharimu Mwalimu wa Shule ya Msingi Kalinzi shilingi 15,000
kwenda Kigoma mjini kuchukua mshahara wake katika Benki ya NMB kila mwezi.
Mwalimu wa shule ya Msingi Miburani, Temeke atatumia shilingi 600 tu kwenda
kuchukua mshahara wake katika Benki ya NMB tawi la Bank House (angeweza
kutembelea kwa mguu kwenda tawi la Temeke pia lakini tuchukulie alikuwa na kazi
mjini vilevile). Hawa ni walimu ambao ni daraja moja, wanalipwa mshahara sawa
lakini uwepo wa barabara (zilizojengwa kwa jasho la mkulima wa kahawa wa
Kalinzi) unampa unafuu huyu masikini wa Temeke, Dar es Salaam na kumkandamiza
katika ufukara Mwalimu wa Kalinzi, Kigoma. Mwaka 2010 barabara ya lami ilifika
Kalinzi. Barabara kubwa ya kwanza mkoani Kigoma toka Uhuru mwaka 1961. Hivi
sasa Mwalimu wa Kalinzi anatumia shilingi 3,000 kwenda Benki. Ahueni kubwa sana
ambayo walimu wengi maeneo vijijini bado hawana. Ahueni aliyosubiri miaka 40
kuipata.
Ukiangalia
Bajeti ya Tanzania utaona namna ambavyo rasilimali kubwa ya nchi inatumika
kutatua changamoto za watu wa mijini na hasa Dar es Salaam. Wabunge (ambao
wengi wetu tunatumia muda mwingi sana Dar es Salaam) bila kujali majimbo au
mikoa yao hukasirikia sana, kwa mfano, foleni Dar es Salaam na kuisukuma
Serikali kutenga fedha zaidi za kujenga barabara za Dar es Salaam. Sasa Dar es
Salaam, kwa kutumia mabilioni ya fedha, zinajengwa barabara za kupaa juu
(flyovers). Umeme ukikatika Dar es Salaam, waandishi wa habari wanaandika ‘nchi
gizani’ bila kujali kuwa Watanzania wa Urughu kule Iramba na wengine
asilimia 83 ya Watanzania wapo kwenye giza la kudumu. Zaidi ya fursa
walizonazo, masikini wa mijini pia sauti zao zinasikika. Mafukara wa Vijijini
nadra kuwasikia.
Tusisahau
jambo hili. Azimio lilisema.
Subscribe to:
Posts (Atom)