1.Uwajibikaji wa kisiasa wa viongozi wa serikali na idara zake.,Waziri
Emmanuel Nchimbi,IGP Mwema,Paul Chagonja,RPC Morogoro na Kamanda wa
FFU,na RPC IRINGA na Kamanda wa FFU wajiuzulu na au wafukuzwe kazi
2.RPC Morogoro na Iringa,makamanda wa FFU Morogoro na Iringa,na
maaskari waliouwa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka
3.Rais aunde tume huru ya uchunguzi wa vifo tata katika matukio ya
kisiasa.1.ARUSHA vifo 3.IGUNGA,vifo vingi havijulikani bado,3.ARUMERU
MASHARIKI,vifo 5, 4.SINGIDA kifo 1, MOROGORO na IRINGA
chadema haitatambua wala kushirikiana na kamati batili ya NCHIMBI.
4.Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa ni mtu hatari kwa taifa kwa
kauli tata anazozitoa.anashirikiana na au anajipendekeza kwa CCM na
Serikali yake.CHADEMA tangu sasa haitafanya kazi na Tendwa wala
kufanya mawasiliano naye ya kiofisi.Labda kama atagundua makosa yake
na kuomba msamaha,chadema itatafakari namna ya kufanya naye kazi tena.
5.TBC TAIFA Television na Redio ni hatari kwa taifa,kwa kubobea
kupotosha umma juu ya matukio mengi.Hivyo CHADEMA Inatangaza mgogoro
na TBC na inaelekeza na kuomba wanachama ,wapenzi,na wananchi wote
wapendao ukweli na haki,kuisusia TBC
6.Jeshi la Polisi lijue kuwa Maandamano ndiyo siasa yenyewe na
mikutano ya hadhara ni lazima kwa mawasiliano ya umma na siasa.kuzuia
vitu hivyo ni kunyima wananchi haki yao ya kikatiba ya uhuru wa
kukusanyika na kutoa maoni,pia kupata habari na taarifa
7.Operesheni MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba
ilivyopangwa katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa
Siku si nyingi.Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo
mojawapo singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki
na baiskeli na miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo
mengine,Chadema wanasema kwa sababu maalum katika jimbo hilo watapita
kitongojikwa kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya viongozi (msisitizo
ni wa msoma MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri
ya wanahabari waliokuwepo)
8.Kutokana na mgogoro wa muda mrefu mkoani mwanza uliosababisha meye
wa chadema kuvuliwa umeya kinyume na utaratibu na kwa njama za CCM na
Serikali,na bahati mbaya sana kwa kushirikisha madiwani wa
CHADEMA,KAMATI KUU imewavua UANACHAMA madiwani wake wawli 1 ADAMU
CHAGULANI wa kata ya IGOMA na HENRY MATATA wa KITANGIRI, PIA uongozi
wote wa CHADEMA mkoa wa mwanza Umevunjwa.
Imesomwa na
Mwenyekiti CHADEMA Taifa
Source: www.wanabidii.net
No comments:
Post a Comment