Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud , amenusurika
jaribio la kumuua mjini Mogadishu.Milipuko miwili imetokea nje la lango la
makao ya rais huyo katika hoteli ya Al-Jazeera wakati rais huyo alipokuwa
anajiandaa kufanya mkutano na waandishi wa habari.Taarifa zinasema kuwa waziri
wa mambo ya nje wa Kenya Sam Ongeri pia alikuwa katika hoteli hiyo wakati wa
shambulizi. Hata hivyo wawili hao wamenusurika. Inaarifiwa watu wanne wameuawa
na wengine watatu kujeruhiwa.
Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
No comments:
Post a Comment