Thursday, October 4, 2012

Meli Ya Utoaji Mimba Yazuiliwa Kuingia Morocco



 
 
 
 
Meli moja ya Uholanzi iliyokuwa ikielekea katika pwani ya Morocco kutoa huduma ya utoaji mimba kwa wanawake imezuiliwa kuingia bandarani kwa mujibu wa wanaharakati walioituma nchini humo. 

Kundi la wanaharakati hao wanawake linasema kuwa bandari ya Smir imefungwa kabisa na meli za kivita zinalinda doria eneo la bandari hiyo.

 Hapo jana Morocco ilisema kuwa meli hiyo haijapewa mualiko na mamlaka zinazotambuliwa nchini humo na hivyo ilikuwa ikifanya shughuli hiyo kinyume cha sheria. Sheria za Morocco zinakataza utoaji mimba isipokuwa tu iwapo maisha ya mwanamke mjamzito yako hatarini. 

 Ibtissame Lachgar, ambaye ni mmoja wa wanaharakati wanaotetea haki ya utoaji mimba amesema wanawake wengi wanalazimika kufanya utoaji mimba kwa njia zisizo rasmi ambazo ni hatari. 

                Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

Sumaye atahamia CHADEMA?


Na: Mussa Juma, Arusha na Boniface Meena,MWANANCHI 

SIKU chache baada ya kushindwa katika uchaguzi wa ndani kwenye nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amekutana na viongozi wa Chadema ikidaiwa kuwa ni kujadili pamoja na mengine, uwezekano wa kuhamia huko ili agombee urais katika Uchaguzi Mkuu ujao 2015.

 Sumaye ambaye anatajwa kuwa alikuwa na mpango wa kuwania urais kupitia CCM, alishindwa katika uchaguzi wa kuwania ujumbe wa Nec, baada ya kupata kura 481 dhidi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk Mary Nagu aliyepata kura 648. 

Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa Chadema, zimeeleza kuwa Sumaye hakuridhishwa na mchakato wa uchaguzi huo wa Nec na kwa matokeo hayo, alikutana na viongozi wa Chadema kujadili mustakabali wake kisiasa. Jana, mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya Chadema, ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alithibitisha Sumaye kukutana na viongozi wa Chadema.

 Hata hivyo alisema hawajafikia mwafaka. Alisema mawasiliano ya Chadema na Sumaye yalianza mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Septemba 30, mwaka huu yaliyomwengua kigogo huyo kwenye kinyang’anyiro hicho.

 “Ni kweli kuna watu wa CCM tumewasiliana nao baada ya uchaguzi ule (wa Nec) na Sumaye tunawasiliana naye pia lakini siwezi kusema tumefikia wapi,” alisema mjumbe huyo na kuendelea: “Suala kwamba amekubaliwa kujiunga na Chadema au la, nadhani huu ni uamuzi wake. Ninachoweza kusema ni kwamba vikao vilikuwepo na vinaendelea kukaliwa.

 Alisema baada ya matokeo ya Hanang’ na hali ya kisiasa ndani ya CCM, Chadema kimekuwa kikiwasiliana na Sumaye na kikubwa ambacho kinajionyesha ni kada huyo wa CCM kutoridhishwa na hali ya mambo ndani ya chama chake. Mjumbe huyo wa Chadema alisema chama hicho Wilaya ya Hanang’ kinaandaa mkutano maalumu wa kuwapokea wanachama wapya wa CCM, wengi wao wakiwa baadhi ya walioanguka kwenye uchaguzi wa Nec wilayani humo. 

Habari zaidi zimeeleza kuwa Chadema kimepanga siku yoyote juma lijalo, kuwapokea wanachama wapya kutoka CCM, baadhi wakiwa wale walioshindwa kwenye uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika wilayani Hanang’. Mmoja wa watu wa karibu na Sumaye alisema anachojua ni kwamba Chadema wanamtaka Sumaye na siyo Sumaye kukitaka chama hicho cha upinzani. 

“Wamekuwa wakimfuatafuata mara nyingi na mazungumzo ya aina hiyo si mageni baina ya Sumaye na Chadema. Ila ninachoweza kusema, safari hii chochote kinaweza kutokea kutokana na hasira alizonazo (Sumaye). Ngoja tusubiri, atafanya mkutano na waandishi Jumapili.” Sumaye, Mbowe wazungumza Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Sumaye alisisitiza kuwa atazungumzia masuala yote yanayohusiana na uchaguzi huo wa Hanang’ atakapokutana na waandishi wa habari, Dar es Salaam.

 “Nitakutana na waandishi wa habari kuzungumzia kilichotokea naomba tu mwendelee kunipa muda,” alisema Sumaye na kuongeza kuwa alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Dar es Salaam. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye si msemaji wa Sumaye... “Sitaki kumzungumzia Sumaye.

Mimi si msemaji wake. Tumsubiri yeye azungumze kuhusu hilo.” Kada wa CCM Hanang’ anena Katika hatua nyingine, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Hanang’, Goma Gwaltu amekionya chama hicho kuwa kisipodhibiti vitendo vya rushwa katika chaguzi zake, kitakufa. Gwaltu alisema jana kwamba kwa mazingira yaliyopo sasa ndani ya CCM bila hatua kali kuchukuliwa, kiongozi asiye na fedha hawezi kushika uongozi na ndiyo sababu anaungana na wana-CCM wengine katika wilaya hiyo, ambao wanafikiria kukihama chama hicho.

 “Kama wewe una nia ya kuendelea na siasa siyo rahisi kushinda hapa Hanang’ ukiwa hukubaliani na watu fulani, sasa mimi naona ni bora tu kutafuta chama kingine kwani siyo dhambi,” alisema Gwaltu bila kuwataja ambao wanataka kuhama CCM. Hata hivyo, Gwaltu alisema kwa upande wake, hafikirii kuendelea na mambo ya siasa wala kulalamika makao makuu ya CCM kuhusiana na alichokiita hujuma alizofanyiwa.

Kikwete Atembelea Canada

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo Jumatano Oktoba 4, 2012
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  kuanza ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo Jumatano Oktoba 4, 2012. Jumba hilo ndilo makazi  na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.

Wednesday, October 3, 2012

Louise na Martine Malaya mapacha wa Masterdam

 
Makahaba hawa wameangaziwa kufuatia kutolewa kwa kumbukumbu zao na Filamu inayohusu maisha yao. Filamu hiyo, (Meet the Fokkens), inawaangazia Makahaba mapacha wenye umri wa miaka 70 Louise na Martine Fokken ambao walitufichulia siri yao katika kufanya ukahaba katika Mji maarufu zaidi kwa ufuska duniani.
Louise na Martine hutumia muda wao mwingi wakiwa kwenye Maskani yao ya vyumba viwili katika eneo la Ijmuiden, magharibi mwa Amsterdam. Huku wakiwa wamevalia viatu vya ndala, wao huranda randa hapa na pale chumbani wakinywa kahawa na kula keki wakionekana kukosa muelekeo.
Martine anaimba kwa sauti ya chini huku Louise akielezea masaibu yaliyoikumba familia yake na kumlazimu kukimbilia usalama wakati wa Vita vya pili vya Dunia.
Mama yao alikuwa na usuli wa Kiyahudi, jambo walilofanya kuwa siri kubwa kwa Wanajeshi wa Nazi waliokuwa wanashika doria nchini Uholanzi. Wimbo wa Louise uligusia Furaha na Huzuni za maisha.
"Tulikuwa watoto wadogo wakati huo wa vita. Ving'ora vilipoanza kulia, mama yetu alituficha katika eneo la chini ya nyumba. hatukuwa na kofia za chuma, hivyo basi tulitumia vikaango vya kupikia kukinga vichwa vyetu. Tulionekana kuchekesha na kana kwamba tunafurahia hali hiyo."
Nilimuuliza iwapo maisha wakati huo hapa Amsterdam, yalikuwa ya furaha au kuhuzunisha?
Makahaba mapacha Louise na Martine
Mapacha hao wanasema kutolewa kwa kumbukumbu zao kumebadilisha muelekeo wao; hapo mbeleni walitusiwa, sasa wanaheshimiwa "Oh ni kicheko, bila shaka ni kicheko. huna budi kucheka hata unapokuwa na huzuni kwa sbabu ni maisha yako na huwezi kuyabadilisha, lakini ni bora ukiwa unatabasamu kila mara."
Dada hao wawili wanatingisa vichwa vya ishara ya kuafikiana katika wanayoeleza.
Hata hivyo, tabasamu lao la kujilazimisha haliepuki kudhihirisha huzuni inayojitokeza machoni mwao.
"Bila shaka hatukuwaza kamwe tulipokuwa na umri wa miaka 14 au 15 kwamba siku moja tungejiingiza kwenye Ukahaba. Tulikuwa wabunifu na tulikuwa na Matarajio maishani" akadokeza Martine says.
Louise naye akaongezea: "kila siku mimi husema ni mume wangu aliyenipiga na kuniingiza kwenye ukahaba. Alikuwa mtu anayetumia mabavu na kutishia kutengana nami endapo ningekataa kufanya ukahaba ili kutafuta pesa.
"Yeye alikuwa kipenzi maishani mwangu…" akasema.
Wanawe Louise' hatimaye wakaishia kulelewa kwenye makao ya watoto. Alituonyesha mojawapo ya picha zilizopo kwenye rafu ya vifaa vya kale, inayodhihirisha nyuso zao zenye tabasamu.
Uzoefu wa miaka mingi
Martine bado anafanya Ukahaba. Anasema malipo ay uzeeni anayopata kutoka kwa Serikali ya Uholanzi hayamtoshelezi kujikimu kimaishai. Isitoshe anaugua ugonjwa wa Baridi yabisi.
Martine anasema ijapokuwa angependa kustaafu lakini hawezi kuendelea kujikimu kimaisha. Filamu inayomuhusu inamuonyesha akiwa kazini, amejipachika kwenye kiti akiwa amevalia soksi ndefu, mshipi na viatu vya kisigino.
Makahaba mapacha Louise na Martine
Martine Fokken ni kivutio kwa wanaume wakongwe badala ya vijana wanaompita bila hata kumtazama na kumkejeli kuwa amezeeka mno. Kama kawaida yake, anaangua kicheko na kusema hajali kamwe.
Anasema nyakati zimebadilika: "Vijana wa sasa ni tofauti, wanakunywa pombe sana, wamenona na hawakuheshimu. Wanapaswa kuwa kwenye pikipiki zao kama wavulana wa Kidachi badala ya kupoteza wakati wakinywa pombe."
Licha ya ushindani mkali kutoka kwa Vidosho wenye umri mdogo katika eneo la karibu, Martine hakosi wateja.
Anaonekana kuwavutia zaidi Wanaume wazee. Yeye hutumia vitu wanavyopendelea kuvaa ili kuwavutia kama vile kuingia kwenye madanguro akiwa na mjeledi huku amevaa viatu vya kisigino kirefu.
Chanzo: BBC

Taswira: Uzuri wa Jiji la Aleppo Syria Kabla ya vita. Sasa ni magofu tu yamebaki. Vita si mchezo.

Taswira: Milipuko minne iliyofuatana kwa dakika chache imetokea leo katika Jiji la Allepo Syris na kuuwa watu takriban 40.



http://www.islamicinvitationturkey.com/wp-content/uploads/2012/05/blast-in-Aleppo-.jpg
Takriban watu 40 wameuawa katika milipuko mitatu ya mabomu yaliyotegwa ndani ya magari katika mji wa Allepo nchini Syria
Mashambulio hayo yametokea katika eneo linalodhibitiwa na majeshi ya serikali. Mashambulio mawili yametokea katikati mwa mji na lingine nje ya ukumbi wa mji huo.
Picha za televisheni zimeonyesha uharibifu mkubwa huku majengo yakiharibiwa na pia barabara. Miili ya watu inabebwa kwa kutumia blanketi.
Mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi yameongezeka mjini Aleppo katika siku za hivi karibuni na kuugawa mji huo mara mbili.
Wapiganaji wa upinzani walianzisha upya mashambulizi wiki iliyopita katika jaribio la kunyakua maeneo zaidi ya mji huo.

AJALI YA MBALIZI MBEYA KIBAKA APEWA KICHAPO NAYE AFA









UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni huo ndio msemo pekee ambao naweza kuutumia katika kukujuza yaliyotokea mapema leo mchana katika ajali mbaya ya Mbalizi Mbeya Vijijini.
Wakati wengine wakiendelea kuokoa majeruhi wengine wamejikuta wakifanya tofauti na vile ilivyotegemewa pale kijana mmoja alipojitoa mhanga na kuingia katika mmojawapo wa waokoaji na kutaka kumchomolea fedha “ waswahili huita mshiko”.

Asalale kijana huyo ambaye hajafahamika jina mpaka mauti yanamkuta katika tukio hilo alikwidwa na mashuhuda wa ajali hiyo na kupewa kichapo cha mbwa mwizi wa kuku.

Wananchi wakichota mafuta kwenye ajali ya mbeya. Hatari tupu


KWELI BINADAMU TUNATOFAUTIANA 
HUKU TANKI LA MAFUTA LIKIENDELEA KUTEKETEA WENGINE WANAENDELEA KUKINGA MAFUTA HATARI TUPU