UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya
Firauni huo ndio msemo pekee ambao naweza kuutumia katika kukujuza yaliyotokea
mapema leo mchana katika ajali mbaya ya Mbalizi Mbeya Vijijini.
Wakati wengine wakiendelea kuokoa
majeruhi wengine wamejikuta wakifanya tofauti na vile ilivyotegemewa pale
kijana mmoja alipojitoa mhanga na kuingia katika mmojawapo wa waokoaji na
kutaka kumchomolea fedha “ waswahili huita mshiko”.
Asalale kijana huyo ambaye
hajafahamika jina mpaka mauti yanamkuta katika tukio hilo alikwidwa na
mashuhuda wa ajali hiyo na kupewa kichapo cha mbwa mwizi wa kuku.
|
No comments:
Post a Comment