Friday, September 7, 2012
ASKARI watano wamekamatwa
ASKARI watano wa Jeshi la Polisi akiwamo anayetuhumiwa kumlipua kwa bomu Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, marehemu Daud Mwangosi wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa na jeshi hilo mkoani Iringa.
Taarifa ya kukamatwa kwa askari hao imekuja siku moja baada ya kubainika kwamba, askari kadhaa walioendesha operesheni dhidi ya wafuasi wa Chadema mkoani Iringa na kusababisha kifo cha Mwangosi walitoka mikoa ya Dodoma, Mbeya na Morogoro.
Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na baadhi ya askari polisi mkoani Iringa na Makao makuu jijini Dares Salaam, zilisema kuwa polisi hao, akiwamo yule aliyeonekana kwenye picha za video na za mnato akimlipua kwa mtarimbo wa bomu la machozi (jina tunalo) wamekamatwa na kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Iringa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment