Friday, September 14, 2012

VITAAAAAA! SYRIA INAKWISHA JAMANI!

Goran Tomasevic's dramatic photos of the fighting around Aleppo in Syria

4 August 2012: A Free Syrian Army fighter gestures as others carry a fighter shot by Syrian Army soldiers during clashes in  Aleppo

4 August 2012: A Free Syrian Army fighter reacts after his friend was shot by Syrian Army soldiers during clashes in Salah al-Din neighbourhood

7 August 2012: .A Free Syrian Army fighter takes cover during clashes with Syrian Army in the Salaheddine neighbourhood of central Aleppo


7 August 2012: A Free Syrian Army fighter screams in pain after he was injured in a leg by shrapnel from a shell fired from a Syrian Army tank in the Salaheddine neighbourhood

11 August 2012: A Free Syrian Army fighter fires an RPG after a Syrian Army tank shell hit a building across a street during heavy fighting

11 August 2012: A Free Syrian Army fighter tries to fix his jammed rifle during a heavy fighting

A Free Syrian Army fighter takes cover in a house during clashes in Aleppo



12 August 2012: A Free Syrian Army fighter helps a woman to run across a street during clashes in Aleppo




12 August 2012: Free Syrian Army fighters take a break from clashes in a coffee shop in Aleppo




13 August 2012: A Free Syrian Army fighter drags a dead man out of the line of sniper fire


14 August 2012: A Free Syrian Army fighter fires his sniper rifle from a house in Aleppo

16 August 2012: Free Syrian Army fighters carry the body of a fellow fighter during clashes in Aleppo
16 August 2012: A Free Syrian Army fighter carries the body of a fellow fighter during clashes in Aleppo

 http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02312/20120816-dead-figh_2312196k.jpg

Machafuko yaendelea katika nchi za kiarabu kupinga filamu inayomkashifu Mtume Mohamad




Waandamanaji walioghadhabishwa na filamu inayodhihaki dini ya kiisilamu wameshambulia balozi za Uingereza na Ujerumani mjini Khartoum, Sudan.
Waandamanaji walianza kuwasha moto na kisha kuichanachana bendera ya Ujerumani na kuweka bango lenye maandiko ya kiisilamu ambapo bendera hiyo ilikuwa.
Taarifa zinazohusiana
Maandamanao yangali yanaendelea katika nchi za Mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika kuilaani filamu ya Marekani inayokejeli Mtume Muhammad.
Mjini Cairo, polisi waliwarushia gesi ya kutoa machozi na kuwatawanya waandamanaji takriban 500,kutoka katika ubalozi wa Marekani.
Maandamano pia yalifanyika katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.
Msemaji wa ubalozi wa Uingereza amethibitisha BBC kuwa maandamano yanafanyika nje ya ubalozi wa Uingereza na kusema kuwa polisi wa Sudan wako katika eneo hilo kudhibiti hali.
Hata hivyo, msemaji huyo hangeweza kuthibitisha ikiwa waandamanaji waliingia katika ubalozi huo au ikiwa maandanamo yana uhusiano wowote na filamu hiyo inayopingwa na waisilamu kote dunian

Njama ya mashambulizi yatibuliwa Kenya





Magwanda ya mabomu ya kujilipua
Polisi nchini Kenya wamenasa magwanda yenye mabomu ya kujilipua pamoja na zana zengine ambazo zilikuwa zitumike kwa mashambulizi ya kigaidi mjini Nairobi.
Washukiwa wawili wamekamatwa katika msako huo uliofanywa asubihi ya leo katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi.

Taarifa zinazohusiana

Msemaji wa polisi nchini Kenya Eric Kiraithe anasema kuwa maguruneti kumi na mbili pamoja na bunduki aina ya AK 47 pia zilinaswa wakati wa msako uliofanywa na polisi mtaani humo.
"tunaamini kuwa silaha hizi zilinuiwa kutumika kufanya mashambulizi ya kigaidi mjini Nairobi'' alisema bwana Kiraithe.
Msako huo uliofanywa na polisi Ijumaa uliongozwa na polisi wa kupambana na ugaidi baada ya polisi kupata habari kutoka kwa raia.
Na baada ya masaa kadhaa ya kuwahoji washukiwa, magwanda manne ya mabomu ya kujitoa mhanga , mabomu mawili na silaha zingine zilipatikana ndani ya nyumba ya mshukiwa mmoja.
Polisi wanaamini kuwa mabomu hayo yalikuwa na vilipuzi vyenye uzito wa kilo arobaini na yangetumika kushambulia baadhi ya sehemu za mji mkuu Nairobi na miji mingine mikubwa.
Bwana Kiraithe amelaumu kundi la Al Shabab. Amesema kuwa washukiwa wengine 8 wako mbioni baada ya washukiwa Abdul majid Mohammed raia mkenya na Suleiman Abdi Aden msomali, kukamatwa na polisi wa Kenya.
Wangali wanahojiwa na polisi na watafikishwa mahakamani baadaye wiki ijayo.
Silaha hizo zinasemekana kufanana na zile zilizotumika katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika nchini Uganda dhidi ya watu waliokuwa wanatazama fainali ya kombe la dunia mwaka 2010, ambapo watu 76 waliuawa
Kundi la Al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi nchini Uganda, wakisema kuwa wanapinga nchi hiyo kujihusisha na harakati dhidi ya kundi hilo nchini Somalia.
Kenya imeshambuliwa karibuni na kundi la al-Shabab baada ya kupeleka vikosi vyake Somalia.

Rais Kikwete Atembelea Kenya

 Rais Kikwete akiangalia kondoo  wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho
 Rais Kikwete akiangalia ng'ombe wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho, n6- Rais Kikwete akiangalia kondoo  wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho, n7- Rais Kikwete akiangalia mchoro wa ujenzi wa jengo la kutengeneza maziwa ya unga wa  kiwanda hicho. Anayemuelekeza ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho Kenyatta,
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake baada ya  kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo  ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.

Mkutano wa CHADEMA UINGEREZA

JE, UNAIPENDA TANZANIA?
KAMA JIBU NI NDIYO, BASI NJOO UUNGANE NASI MILTON KEYNES
NJOO UWE SEHEMU YA HISTORIA
NETHERFIELD  MEETING PLACE, FARNBOROUGH NETHERFIELD
MK6 4JB kuanzia saa kumi jioni mpaka saa tatu usiku
NJOO UJIUNGE NA MFUKO WA DHARURA
AKINA MAMA NJOONI MJIUNGE NA JUMUIYA YA WANAWAKE CHADEMA 

Kutakuwa na usafiri kutoka London na Reading
REFRESHMENTS WILL BE AVAILABLE
kwa taarifa zaidi, tafadhaliwasiliana na wafuatao:- 

Mwenyekiti: Mr CHRIS LUKOSI - 
07903828119
&
Mwakilishi wa Reading: Mr GERALD LUSINGU 
PEOPLE'S POWER!
 
Souece: Haki Ngowi
Wananchi wa Sumbawanga wakimshangaa ng'ombe aliyekuwa juu ya paa la kwao leo asubuhi. Ngombe huyo amekuwa akila mazao ya watu mara kwa mara
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Seif Sharif Hamad, siku ya Alhamisi tarehe 14/9/12 alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia maswala ya Afrika Bw. Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao walibadilishana mawazo kuhusu maswala ya Tanzania na hususan hali ya kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo hayo yalihudhuria na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Peter Kallaghe
 Makamu wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akisalimiana na Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya ya Waingereza walio wahi kuishi Tanzania (Britain Tanzania Society). Aliyepewa mkono na Mheshimiwa Makamu wa Rais ni Bwana  David Brewin Mhariri wa Jarida la kila mwezi linalotolewa na BTS,  Mama Liz Fennell, Makamu wa Rais BTS (mbele kulia), Mama Valerie Leach - Katibu (kwanza kushoto), Bwana Dan Coo-  Mwanachama BTS, Bwana Ron Fennel, Afisa wa Miradi ya BTS kwa Tanzania na Bwana Andrew Coulson, Afisa Mkuu wa Mipango ya Jumuiya hiyo ya BTS.
 
 
 Makamu wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akisalimiana na Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya ya Waingereza walio wahi kuishi Tanzania (Britain Tanzania Society). Aliyepewa mkono na Mheshimiwa Makamu wa Rais ni Bwana  David Brewin Mhariri wa Jarida la kila mwezi linalotolewa na BTS,  Mama Liz Fennell, Makamu wa Rais BTS (mbele kulia), Mama Valerie Leach - Katibu (kwanza kushoto), Bwana Dan Coo-  Mwanachama BTS, Bwana Ron Fennel, Afisa wa Miradi ya BTS kwa Tanzania na Bwana Andrew Coulson, Afisa Mkuu wa Mipango ya Jumuiya hiyo ya BTS.
 
 
 
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akiwa pamoja na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki. Mheshimiwa Seif alikutana na Mabalozi hao jana kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London. Katikati ya picha ni Mheshimiwa, Makamu wa Rais, Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Kallaghe (kushoto), Balozi wa Rwanda, Mheshimiwa Ernest Rwamucyo (Pili kushoto), Balozi wa Uganda, Mheshimiwa Joan Rwabyomere (Pili kulia), na Balozi Mdogo wa Burundi, Mheshimiwa Bernard Ntahiraja (Kwanza kulia).
--
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, aliendelea na Ziara yake ya jana hapa nchini Uingereza. Mheshimwa Seif, jana alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia maswala ya Afrika Bw. Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao walibadilishana mawazo kuhusu maswala ya Tanzania na hususan hali ya kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe. Vile vile Mheshimiwa Makamu wa Rais, aliweza kukutana na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki na Viongozi wa Jumuiya ya Waingereza waliowahi kuishi Tanzania, ijulikanayo kama Britain Tanzania Society (BTS).

Leo hii siku ya Ijumaa, Jioni, kuanzia Saa 18:00pm mpaka saa 21:00, Mheshimiwa Makamu wa Rais atakutana na Watanzania wote waishio London, katika Ukumbi wa University of London Union, Mtaa wa Malet Street, WC1E 7HY

Watanzania wote wenye nafasi ya kufika mnakaribishwa.

Watakao hudhuria mnaombwa sana kuzingatia muda uliopangwa.
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Wateja,Mussa Ramadhan Haji,kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji (ZAWA) ikiwa ni miongoni waliochagia katika ujenzi wa   Kituo cha Polisi cha Fumba Mkoa Mjini Magharibi,wakati wa hafla ya ufunguzi wa kituo hicho jana.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wenyeji wake wa Chuo Kikuu cha Kenyatta baada ya kufungua Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.Picha na IKULU

  Rais jakaya kikwete akiweka shada la maua kwenye kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta    jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo  ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  na Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta    jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo  ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.

Thursday, September 13, 2012

ZITTO: TUSISAHAU JAMBO HILI-AZIMIO LILISEMA




 
Unyonyaji wa ‘wamjini’ dhidi ya ‘wavijijini’ – Tusisahau jambo hili

Zitto Kabwe, Mb

Mnamo tarehe 12 Septemba, 2012 niliandika makala iliyochapwa kwenye magazeti mawili nchini, Raia Mwema na Tanzania Daima. Makala hiyo ‘Mafukara milioni 30, Mabilioni 30’ ilikuwa inaonyesha namna ambavyo mfumo wa uchumi wa nchi yetu ni wa kinyonyaji. Kwamba wakazi wa mijini wanafaidi zaidi rasilimali za nchi kuliko wakazi wa Vijijini. Vilevile nilieleza kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania ni wa kifisadi na ufisadi unafaidisha kikundi kidogo cha watu mijini au wenye tabia za kimjini na hivyo kukosesha huduma za msingi za wananchi wengi waishio vijijini. Mwanazuoni kijana Sabatho Nyamsenda ameandika uchambuzi wake mzuri kuhusu makala hiyo kama ‘Tangazo la Coca Cola na wito wa Zitto dhidi ya Vizito’ ambapo amejaribu kuonyesha kuwa masikini wa mijini ni sawa tu na mafukara wa vijijini. Sikubaliani naye. Nitatumia Azimio la Arusha kuboresha hoja yangu na pia mfano halisi wa Mwalimu wa Kalinzi, Kigoma dhidi ya Mwalimu wa Miburani, Temeke.

Muono wangu unathibitishwa na mambo matatu. Kwanza ni kuongezeka kwa kasi kwa tofauti ya kipato kati ya walionacho na wasionacho ambapo sasa kuna kundi dogo la watu ni matajiri sana na kundi kubwa sana ni mafukara sana. Nilionyesha kuwa asilimia 30 ya Watanzania wanamiliki asilimia 75 ya Pato la Taifa. Pili, nilionyesha kuwa kasi ya kupunguza umasikini nchini inaonekana mijini kuliko vijijini ambapo katika kipindi cha miaka 16, umasikini wa watu wa Dar es Salaam, kwa mfano, umepungua kwa asilimia 12 wakati umasikini vijijini umepungua kwa asilimia 2 tu. Tatu, nimeonyesha kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa vijijini ipo chini ya wastani wa ukuaji wa uchumi wa Taifa kutokana na sekta ya Kilimo ambayo inaajiri asilimia 75 ya Watanzania imekuwa ikikua ‘flatlining’ kwa asilimia 4 wakati Uchumi wa nchi umekuwa ukikua kwa wastani wa asilimia 7 katika muongo mmoja uliopita.

Nilionyesha kuwa tabaka la chini la watu wa mijini ni masikini kwani wamepewa fursa za kuweza kuondokana na umasikini wakati watu wa vijijini ni mafukara kwani mfumo kwa makusudi umewanyima fursa. Kimombo ninasema watu wa tabaka la chini la mijini ni ‘poor’ na watu wa vijijini ni ‘impoverished’. Azimio la Arusha limeonyesha muono kama huu na lilionya kutosahau mwono huu katika andiko lake. Ninanukuu.

"Vile vile mkazo wa fedha na wa viwanda unatufanya tukazanie zaidi maendeleo ya mijini. Tunatambua kuwa hatuwezi kupata fedha za kutosha kuleta maendeleo katika kila kijiji na ambayo yatamfaa kila mwananchi. Tunajua pia kuwa hatuwezi kujenga kiwanda katika kila kijiji ili kisaidie kuleta maendeleo ya fedha na viwanda katika kila kijiji; jambo ambalo tunajua kuwa haliwezekani. Kwa ajili hiyo, basi, fedha zetu huzitumia zaidi katika miji na viwanda vyetu pia hujengwa katika miji. Na zaidi ya fedha hizi huwa ni mikopo. Japo zijenge shule, hospitali, majumba au viwanda ni fedha za mikopo. Hatimaye lazima zilipwe.
Lakini ni dhahiri kwamba haziwezi kulipwa kwa fedha zinazotokana na maendeleo ya mijini au maendeleo ya viwanda. Hazina budi zilipwe kwa fedha tunazopata kutokana na vitu tunavyouza katika nchi za nje. Kutokana na viwanda vyetu hatuuzi na kwa muda mrefu sana hatutauza vitu vingi katika nchi za nje. Viwanda vyetu zaidi ni vya kutusaidia kupata vitu hapa hapa ambavyo mpaka sasa tunaviagiza kutoka nchi za nje. Itapita miaka mingi kabla ya kuweza kuuza katika nchi za nje vitu vinavyotokana na viwanda vyetu. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba fedha tutakazotumia kulipa madeni haya ya mikopo ya fedha kwa maendeleo na viwanda mijini hazitatoka mijini na wala hazitatokana na viwanda. Zitatoka wapi, basi? Zitatoka vijijini na zitatokana na KILIMO. Maana ya ukweli huu ni nini? Ni kwamba wale wanaofaidi maendeleo yanayotokana na fedha tunazokopa sio kwa kweli watakaozilipa. Fedha zitatumika zaidi katika miji lakini walipaji watakuwa zaidi ni wakulima.

Jambo hili linafaa kukumbukwa sana, maana kuna njia nyingi za kunyonyana. Tusisahau hata kidogo kwamba wakaaji wa mijini wanaweza wakawa wanyonyaji wa jasho la wakulima wa vijijini. Hospitali zetu kubwa zote ziko katika miji. Zinafaidia sehemu ndogo sana ya wananchi wa Tanzania. Lakini kama tumezijenga kwa fedha za mkopo walipaji wa mkopo huo ni wakulima, yaani wale ambao hawafaidiwi sana na hospitali hizo. Mabarabara ya lami yako katika miji, kwa faida ya wakaaji wa mijini na hasa wenye magari. Kama mabarabaraba hayo tumeyajenga kwa fedha za mikopo walipaji ni wakulima; na fedha zilizonunua magari yenyewe zilitokana na mazao ya wakulima. Taa za umeme, maji ya mabomba, mahoteli na maendeleo mengine yote ya kisasa yako zaidi katika miji. Karibu yote yametokana na fedha za mikopo na karibu yote hayana faida kubwa kwa mkulima, lakini yatalipwa kwa fedha zitakazotokana na jasho la mkulima.

Tusisahau jambo hili. Japo tunapotaja unyonyaji hufikiria mabepari, tusisahau kuwa bahari ina samaki wengi. Nao hutafunana. Mkubwa humtafuna mdogo na mdogo naye humtafuna mdogo zaidi. Katika nchi yetu twaweza kugawa wananchi kwa njia mbili. Mabepari na Makabaila upande mmoja; na wafanyakazi na wakulima upande mwingine. Pia twaweza tukagawa wakaaji wa mijini upande mmoja na wakulima wa vijijini upande mwingine. Tusipoangalia tutakuja kugundua kuwa wakaaji wa mijini nao ni wanyonyaji wa wakulima.” Azimio la Arusha,1967. (msisitizo ni wangu).

Azimio la Arusha limerudia zaidi ya mara moja “Tusisahau jambo hili” ama “Jambo hili linapaswa kukumbukwa sana”. Tumesahau jambo hili. Licha ya kwamba sisi wanasiasa wa kisasa tunaona Azimio la Arusha ni nyaraka “outdated” ipo siku tutakumbushwa kwa njia ambayo hatutakuja kuisahau. Sitaki tufike huko. Mwangwi wa “tusisahau jambo hili” lazima uendelee kutuonyesha kuwa kuna kazi ya kufanya kuhusu Mafukara milioni thelathini wanaoishi kwenye vijiji vyetu. Watanzania hawa wa vijijini hawana fursa za barabara, maji, umeme na hata huduma za jamii kama wenzao wa mijini.

Nitatoa mfano mmoja kuonyesha tofauti ya Masikini wa mjini na Fukara wa kijijini. Wakati nachaguliwa kuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini (jimbo la vijijini) mwaka 2005, ilikuwa inamgharimu Mwalimu wa Shule ya Msingi Kalinzi shilingi 15,000 kwenda Kigoma mjini kuchukua mshahara wake katika Benki ya NMB kila mwezi. Mwalimu wa shule ya Msingi Miburani, Temeke atatumia shilingi 600 tu kwenda kuchukua mshahara wake katika Benki ya NMB tawi la Bank House (angeweza kutembelea kwa mguu kwenda tawi la Temeke pia lakini tuchukulie alikuwa na kazi mjini vilevile). Hawa ni walimu ambao ni daraja moja, wanalipwa mshahara sawa lakini uwepo wa barabara (zilizojengwa kwa jasho la mkulima wa kahawa wa Kalinzi) unampa unafuu huyu masikini wa Temeke, Dar es Salaam na kumkandamiza katika ufukara Mwalimu wa Kalinzi, Kigoma. Mwaka 2010 barabara ya lami ilifika Kalinzi. Barabara kubwa ya kwanza mkoani Kigoma toka Uhuru mwaka 1961. Hivi sasa Mwalimu wa Kalinzi anatumia shilingi 3,000 kwenda Benki. Ahueni kubwa sana ambayo walimu wengi maeneo vijijini bado hawana. Ahueni aliyosubiri miaka 40 kuipata.

Ukiangalia Bajeti ya Tanzania utaona namna ambavyo rasilimali kubwa ya nchi inatumika kutatua changamoto za watu wa mijini na hasa Dar es Salaam. Wabunge (ambao wengi wetu tunatumia muda mwingi sana Dar es Salaam) bila kujali majimbo au mikoa yao hukasirikia sana, kwa mfano, foleni Dar es Salaam na kuisukuma Serikali kutenga fedha zaidi za kujenga barabara za Dar es Salaam. Sasa Dar es Salaam, kwa kutumia mabilioni ya fedha, zinajengwa barabara za kupaa juu (flyovers). Umeme ukikatika Dar es Salaam, waandishi wa habari wanaandika ‘nchi gizani’ bila kujali kuwa Watanzania wa Urughu kule Iramba  na wengine asilimia 83 ya Watanzania wapo kwenye giza la kudumu. Zaidi ya fursa walizonazo, masikini wa mijini pia sauti zao zinasikika. Mafukara wa Vijijini nadra kuwasikia.

Tusisahau jambo hili. Azimio lilisema.

https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gif