Anaonekana Baba Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini mara tu baada ya kukagua gari litakalo tumika kubebe mwili wa marehemu Kardinali Rugambwa
Muonekano wa ndani ya Gari.
Muonekano wa gari litakalo ubeba mwili wa Marehemu Kardinali Rugambwa likiwa tayari limepambwa Maua.
Mtangazaji wa kipindi cha dini, TBC katika kuwajibika
Mzee Dioniz Malinzi akiteta jambo na Askofu Kilaini.
Kila baada ya muda ndivyo wanavyozidi kuwasili Viongozi mbalimbali wa dini .
Kikundi cha Ngoma kutoka nchini Burundi kikiendelea na mashamsham katika mahadhimisho haya.
Shamrashamra za hapa na pale zikiendelea.
Wadau na waumini wakikiristo wakifurahia burudani ya ngoma kutoka Nchini Burundi.
kuelekea ndani ya kanisa kuu.
Mwili ukiingizwa ndani ya kanisa kuu katoliki Jimbo la Bukoba
Heshima ya mwisho katika katika ktabaruku mwili wa Kardinali.
Hapa nashindwa nielezeje ingawa naamini ni mwanzo
wa ukurasa mwingine katika kuendeleza historia ya Marehemu Kardinal
Rugambwa.
Monekano wa kaburi jipya ndani ya kanisa kuu, na pembeni yake zipo kaburi nyingine tatu.
MISA IMEONGOZWA NA ASKOFU MKUU JIMBO LA MWANZA YDATHADEI RUAICH NA KUSAIDIWA NA NESTORIUS TIMANYWA.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda mara tu baada ya kuwasili mjini bukoba
Watu na matukio,hapa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwajibika
Watu walioandaliwa maalum wakiwa wamebeba jeneza lililo na masalia ya
Kardinali Laurean Rugambwa yatari kuingizwa katika Kanisa Kuu la Jimbo
la Bukoba, la Bikira Maria wa Huruma kwa maziko.
Jeneza hilo lilokuwa na masalia likiwa limebebwa juu.
Na Theonestina Juma, Bukoba
MAELFU ya waumini wa Kanisa
Katoliki kutoka ndani na nje ya nchi wamejitokeza kushiriki maziko rasmi ya
masalia ya Kardinali wa Kwanza Mwafrika,Laurean Rugambwa yaliofanyika jana mjini
Bukoba.
Misa ya kuombea masalia ya Kardinali huyo yalioongozwa na Askofu Mkuu
wa Jimbo Kuu la Mwanza,Mhashamu Jude Thadeus Ruwa'ichi, katika Parokia ya
Kashozi alikokuwa amezikwa kwa muda kutokana na Kanisa kuu la Bukoba la Bikira
Maria wa Huruma aliloanza kujenga mwenyewe akiwa hai na kutaka azikwe lilikuwa likifanyiwa ukarabati mkubwa uliochukua
takribani miaka 10.
Katika misa hiyo ilioendeshwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu
la Mwanza, Mhashamu Jude Thadeus Ruwa’ichi yamehudhuriwa na maaskofu zaidi ya 30
kutoka katika majimbo mbali mbali hapa nchini pamoja na miamia ya mapadri pamoja
na watawa
Katika parokia ya Kashozi kutokana na uwingi wa watu waliojitokeza
kushiriki katika misa ya ililazimika geti la kuingilia kanisani kufungwa kwa
muda kwa kuhofia kungeweza kutokea watu kukanyagana, ambapo geti hilo
lilifunguliwa wakati wa kukominika.
"Naomba geti la lango kuu lililokuwa
limefungwa lifunguliwe kwani kwa sasa ni wakati wa kukomunika"alisikika Padri
mmoja akitoa maelekezo.Akihubiri katika misa hiyo ya kuhamisha masalia ya
Kardinali Rugambwa,Mhashamu Ruwa'ichi alisema kila Askofu wa jimbo wa Kanisa
hilo wanayo haki ya kuchagua azikwe wapi.
Alisema hata Kardinali Rugambwa
angependekeza azikwe Jijini Dar Es Salaam alikofanyia kazi za kiuchungaji kwa
miaka mingi ingetekelezwa, lakini kwa hiari na utashi wake alitaka azikwe Bukoba
hivyo ni haki yake.
"Kila Askofu anawajibu wa kuchagua azikwe wapi, naye
Kardinali Rugambwa alitaka azikwe Katika Kanisa Kuu la Bukoba, ni haki yake na
hatimaye leo tunahamisha masalia yake na kwenda kuzika rasmi"alisema Askofu
Ruwa'ichi.
Alisema kuhifadhiwa rasmi masalia yake katika kanisa hilo yatakuwa
yakiombewa na waumini kutoka katika maeneo mbali mbali kutokana na jinsi
alivyokuwa akithamini dini na kumtumikia Mungu.Alisema kupumzishwa si kwamba ni
mahali pake bali ni sehemu alikoandaliwa na Mungu.
Alisema kazi kubwa ya
Kardinali Rugambwa ilikuwa ni kuwaelekeza watu njia ya kwenda kwa Yesu.
Alisema
katika mafundisho hayakuwa porojo bali alieneza habari njema za kumpenda,
kumtumikia Mungu.
Hata hivyo baada ya misa hiyo yalianza maandamano ya magari
na pikipiki ambayo yaliongozwa na Jeshi la polisi Mkoani Kagera ambapo
maandamano hayo yalifika Bukoba mjini saa 9.00 alasiri huku jeneza lililobeba la
Masalia yake likiwa la kifahari lenye namba ya usajili,T 607 BYX
Masalia ya
Kardinali Rugambwa yaliwekwa karibuni saa 4.20 jioni na watu maalum waliokuwa
wameandaliwa.
Aidha katika maziko hayo rasmi katika eneo la kaburi walioenda
ni waandishi wa habari, maaskofu na baadhi ya mapadri waliokuwa na shughuli
maalum pekee.
Askofu Ruwa’ichi aliwaongoza baadhi ya maaskaofu kuweka mashada
ya maua katika kaburi la Kadinali Rugambwa, ambapo katika eneo alikozikwa jumla
kuna makaburi matatu.
Hata hivyo katika mazishi hayo hayakuweza kuwahiwa na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo yeye alitua mjini hapa saa 4.30 jioni wakati
maziko hayo yalianza saa 9.30 alasiri na saa 4.20 akapumzishwa katika nyumba
yake ya milele.
Kutokana na uwingi wa watu waliofurika katika maziko hayo
mjini hapa, magari yote yalioamuriwa kwenda kuegeshwa katika uwanja wa Kaitaba
kulingana na maelezo yaliotolewa na Jeshi la polisi, ambapo hata watu waliokuwa
wakiuza bidhaa mbali mbali walialimika kuuza zaidi ya mita 500 kutoka katika
eneo la sherehe hizo.
Katika sherehe za maziko hayo wanaumini waliweza kushudia moja kwa moja
kupitia screen za lungina zilizokuwa zimewekwa kila sehemu katika
viwanja vya makanisa hayo, Kashozi na Bukoba mjini.
Hata hivyo idadi ya watu waliokuwa nje ya uwanja wa
kanisa hilo waliokosa nafasi ya kukaa ilikuwa sawa na watu waliokuwa ndani ya
viwanja vya kanisa hilo.
Kardinali Rugambwa alizaliwa Julai 12, 1912 katika kijiji cha Bukongo
Rutabo Kamachumu wilayani Muleba katika familia ya kifalme na kufariki dunia
mwaka 1997 akiwa na miaka 85.