Sunday, October 7, 2012

Kardinali Rugambwa azikwa mara ya pili Bukoba

Anaonekana Baba Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini mara tu baada ya kukagua gari litakalo tumika kubebe mwili wa marehemu Kardinali Rugambwa
 Muonekano wa ndani ya Gari.
Muonekano wa gari litakalo ubeba mwili wa Marehemu Kardinali Rugambwa likiwa tayari limepambwa Maua.
 Mtangazaji wa kipindi cha dini, TBC katika kuwajibika
 Mzee Dioniz Malinzi akiteta jambo na Askofu Kilaini.
 Kila baada ya muda ndivyo wanavyozidi kuwasili Viongozi mbalimbali wa dini .
 Kikundi cha Ngoma kutoka nchini Burundi kikiendelea  na mashamsham  katika mahadhimisho haya.
 Shamrashamra za hapa na pale zikiendelea.
 Wadau na waumini wakikiristo wakifurahia burudani ya ngoma kutoka Nchini Burundi.

kuelekea ndani ya kanisa kuu.

 Mwili ukiingizwa ndani ya kanisa kuu katoliki Jimbo la Bukoba

 Heshima ya mwisho katika katika ktabaruku mwili wa Kardinali.
 Hapa nashindwa nielezeje ingawa naamini ni mwanzo wa ukurasa mwingine  katika kuendeleza  historia ya Marehemu Kardinal Rugambwa.


Monekano wa kaburi jipya ndani ya kanisa kuu, na pembeni yake zipo kaburi nyingine tatu.

 MISA IMEONGOZWA NA ASKOFU MKUU JIMBO LA MWANZA YDATHADEI RUAICH NA KUSAIDIWA NA NESTORIUS TIMANYWA.


Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda mara tu baada ya kuwasili mjini bukoba
 Watu na matukio,hapa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwajibika
 Watu walioandaliwa maalum wakiwa wamebeba jeneza lililo na masalia ya Kardinali Laurean Rugambwa yatari kuingizwa katika Kanisa Kuu la Jimbo la Bukoba, la Bikira Maria wa Huruma kwa maziko.




Jeneza hilo lilokuwa na masalia likiwa limebebwa juu.

Na Theonestina Juma, Bukoba
MAELFU ya waumini wa Kanisa Katoliki kutoka ndani na nje ya nchi wamejitokeza kushiriki maziko rasmi ya masalia ya Kardinali wa Kwanza Mwafrika,Laurean Rugambwa yaliofanyika jana mjini Bukoba.
Misa ya kuombea masalia ya Kardinali huyo yalioongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza,Mhashamu Jude Thadeus Ruwa'ichi, katika Parokia ya Kashozi alikokuwa amezikwa kwa muda kutokana na Kanisa kuu la Bukoba la Bikira Maria wa Huruma aliloanza kujenga mwenyewe akiwa hai na kutaka azikwe lilikuwa likifanyiwa ukarabati mkubwa uliochukua takribani miaka 10.
Katika misa hiyo ilioendeshwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Jude Thadeus Ruwa’ichi yamehudhuriwa na maaskofu zaidi ya 30 kutoka katika majimbo mbali mbali hapa nchini pamoja na miamia ya mapadri pamoja na watawa
Katika parokia ya Kashozi kutokana na uwingi wa watu waliojitokeza kushiriki katika misa ya ililazimika geti la kuingilia kanisani kufungwa kwa muda kwa kuhofia kungeweza kutokea watu kukanyagana, ambapo geti hilo lilifunguliwa wakati wa kukominika.
"Naomba geti la lango kuu lililokuwa limefungwa lifunguliwe kwani kwa sasa ni wakati wa kukomunika"alisikika Padri mmoja akitoa maelekezo.Akihubiri katika misa hiyo ya kuhamisha masalia ya Kardinali Rugambwa,Mhashamu Ruwa'ichi alisema kila Askofu wa jimbo wa Kanisa hilo wanayo haki ya kuchagua azikwe wapi.
Alisema hata Kardinali Rugambwa angependekeza azikwe Jijini Dar Es Salaam alikofanyia kazi za kiuchungaji kwa miaka mingi ingetekelezwa, lakini kwa hiari na utashi wake alitaka azikwe Bukoba hivyo ni haki yake.
"Kila Askofu anawajibu wa kuchagua azikwe wapi, naye Kardinali Rugambwa alitaka azikwe Katika Kanisa Kuu la Bukoba, ni haki yake na hatimaye leo tunahamisha masalia yake na kwenda kuzika rasmi"alisema Askofu Ruwa'ichi.
Alisema kuhifadhiwa rasmi masalia yake katika kanisa hilo yatakuwa yakiombewa na waumini kutoka katika maeneo mbali mbali kutokana na jinsi alivyokuwa akithamini dini na kumtumikia Mungu.Alisema kupumzishwa si kwamba ni mahali pake bali ni sehemu alikoandaliwa na Mungu.
Alisema kazi kubwa ya Kardinali Rugambwa ilikuwa ni kuwaelekeza watu njia ya kwenda kwa Yesu.
Alisema katika mafundisho hayakuwa porojo bali alieneza habari njema za kumpenda, kumtumikia Mungu.
Hata hivyo baada ya misa hiyo yalianza maandamano ya magari na pikipiki ambayo yaliongozwa na Jeshi la polisi Mkoani Kagera ambapo maandamano hayo yalifika Bukoba mjini saa 9.00 alasiri huku jeneza lililobeba la Masalia yake likiwa la kifahari lenye namba ya usajili,T 607 BYX
Masalia ya Kardinali Rugambwa yaliwekwa karibuni saa 4.20 jioni na watu maalum waliokuwa wameandaliwa.
Aidha katika maziko hayo rasmi katika eneo la kaburi walioenda ni waandishi wa habari, maaskofu na baadhi ya mapadri waliokuwa na shughuli maalum pekee.
Askofu Ruwa’ichi aliwaongoza baadhi ya maaskaofu kuweka mashada ya maua katika kaburi la Kadinali Rugambwa, ambapo katika eneo alikozikwa jumla  kuna makaburi matatu.
Hata hivyo katika mazishi hayo hayakuweza kuwahiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo yeye alitua mjini hapa saa 4.30 jioni wakati maziko hayo yalianza saa 9.30 alasiri na saa 4.20 akapumzishwa katika nyumba yake ya milele.
Kutokana na uwingi wa watu waliofurika katika maziko hayo mjini hapa, magari yote yalioamuriwa kwenda kuegeshwa katika uwanja wa Kaitaba kulingana na maelezo yaliotolewa na Jeshi la polisi, ambapo hata watu waliokuwa wakiuza bidhaa mbali mbali walialimika kuuza zaidi ya mita 500 kutoka katika eneo la sherehe hizo.
Katika sherehe za maziko hayo wanaumini waliweza kushudia moja kwa moja kupitia screen za lungina zilizokuwa zimewekwa kila sehemu katika viwanja vya makanisa hayo, Kashozi na Bukoba mjini.
Hata hivyo idadi ya watu waliokuwa nje ya uwanja wa kanisa hilo  waliokosa nafasi ya kukaa ilikuwa sawa na watu waliokuwa ndani ya viwanja vya kanisa hilo.
Kardinali Rugambwa alizaliwa  Julai 12, 1912 katika kijiji cha Bukongo Rutabo Kamachumu wilayani Muleba katika familia ya kifalme na kufariki dunia mwaka 1997 akiwa na miaka 85.

No comments:

Post a Comment