Saturday, September 29, 2012

Rais Jakaya Kikwete Aagana na Mabalozi wa Cuba na iran Ikulu Jijini Dar es Salaa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Cuba  nchini Tanzania aliyemaliza muda wake  Mhe Ernesto Gomes Dias  Septemba 28,  2012 Ikulu jijini DAr es salaam Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Iran nchini Tanzania aliyemaliza muda wake  Mhe Mohsen Movahhedi Ghomi  Septemba 28, 2012  Ikulu Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Cuba  nchini Tanzania aliyemaliza muda wake  Mhe Ernesto Gomes Dias  Septemba 28,  2012 Ikulu jijini DAr es salaam Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na na Balozi wa Cuba  nchini Tanzania aliyemaliza muda wake  Mhe Ernesto Gomes Dias Septemba 28,  2012 Ikulu jijini Dar es salaam Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Iran nchini Tanzania aliyemaliza muda wake  Mhe Mohsen Movahhedi Ghomi  Septemba 28, 2012  Ikulu Dar es salaam.Picha na IKULU

Friday, September 28, 2012

Majeshi ya Kenya yaingia Kismayo Kwa kishindo






Kanali Oguna: Msemaji wa Majeshi ya Kenya huko Somalia


Helkopta ya jesi la Kenya ilifanya mashambilizi ya anga


 
Hawa ndio Al Shabaab wanaotafutwa
Maelfu ya raiya wakikimbia makazi yao


Wanajeshi wa kenya waliouwawa hapo nyuma




Mogadishu - Kenya askari walianzisha mashambulizi kabla ya alfajiri ya mji wa bandari wa Kismayu Somalia leo Ijumaa katika shambulio kuendesha al-Qaeda wanaohusishwa na kundi la al Shabaab hii ikiwa ni  ngome yake ya mwisho kubwa.

Mapambano ya makombora yalifanyika mapema leo katika fukwe za Kismayo, walisema wakaaji na waasi wa al shabaab
Kupoteza bandari ya Kismayo inaonekana kuwa pigo kubwa sana kwa Al-shabaab kwa kuwa walikuwa wakitumia bandari hii tangu mwaka 2007 kama njia yao kuu ya mapato

Msemaji wa Jeshi la Kenya Kanali Oguna Koreshi amesema askari wa Kenya na wale wa serikali ya Somalia wamevamia mji wa Kismayu kutoka kaskazini, kusini na baharini kwa wakati mmoja na kuweza kudhibiti sehemu kubwa ya mji wa Kismayo. Askari hao wanaongozwa kwa angani na ndege za kijeshi ambazo zinatoa taarifa zote za kijeshi. Hata hivyo wanajeshi wa Kenya hadi sasa wamekutana na upinzani mdogo sana. Wananchi wanaoishi Kismayu wanashuhudia mapigano karibu kabisa na jiji la kismayo takriban kilometa 2 (maili 2.5) nje ya jiji na wanaona madege ya kivita yakipita juu ya anga la Kismayo.

"Tuliona meli saba mapema asubuhi na sasa wanarusha makombora  yao yanayoonekana  kama umeme wa radi. Al Shabaab wameelekea pwani kupambana nao pwani. Meli zimemwaga askari wengi wa AU ufukweni” Ismail Suglow aliiambia Reuters.

Wenyeji alisema wafanyabiashara walikuwa wamefunga biashara zao na kukimbia. Baadhi ya wanaume walivalia kininja wanaonekana wakichungulia kutoka madirishani mwa nyumba zao.
Habari kwa Hisani ya Reuters: (translated by Fortunato Bahati)


WAMACHINGA WAJIGAWIA VIWANJA NA KUJENGA VIBANDA VYA KUENDESHA BIASHARA ZAO MJINI ARUSHA

Vibanda vya wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) walivyojenga baada ya kuvamia na kujipimia maeneo. Hapa vibanda hivyo vinaonekana kuwa tayari kwa biashara zao.
Wanamama wanaouza mboga mboga ambao walikuwa sehemu ya Wamachinga waliovamia uwanja huo, wakiendelea na biashara zao baada ya kujigawia maeneo.
Wamachinga jiji la Arusha waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Wamachinga jiji la Arusha waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Wamachinga jiji la Arusha waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Polisi wakiwa kwenye magari yao baada ya kufika, kuegesha magari yao upande wa pili wa barabara kwenye kituo cha mafuta kwa muda, kisha kuondoka bila kutawanya wafanyabiashara wago (Wamachinga) waliovamia na kujitwalia eneo hilo.
Polisi wakiwa kwenye magari yao wakifika na kuyaegesha magari yao upande wa pili wa barabara kwenye kituo cha mafuta kwa muda kabla ya kuondoka bila kufanya juhudi zozote za kuwazuia machinga hao kujitwalia eneo hilo.Picha na Grace Macha-
----
Na Mahmoud Ahmad-Arusha

 Hali si shwari katika jiji la Arusha na viunga vyake baada ya wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga kuzua tafrani mara walipovamia eneo la kiwanja cha Ermoil lililopo mkabala na soko la Kilombero na kisha kuanza kugawana maeneo ya kufanyia biashara kwa kujipimia.

Vurugu hizo zimetokea jana wakati Rais Jakaya kikwete akiwa jijini Arusha kufungua mkutano mkubwa wa mapinduzi ya kijani ambao umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka nchi za Afrika,Amerika,Ulaya na Asia. Hatahivyo,katika vurugu hizo mfuasi mmoja wa chama cha     wananchi(Cuf),Athuman Abrahaman alishambuliwa kwa mawe na kisha kujeruhiwa eneo la usoni na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chadema huku gari la matangazo la Cuf nalo likijikuta likipopolewa kwa mawe na spika zake kuharibika vibaya. Askari wa jiji la Arusha walionekana majira ya saa 3;30 asubuhi akipita na gari lao katika maeneo mbalimbali ya jiji hapa huku wakiwatangazia wamachinga wote kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia biashara zao. 

Askari hao walikuwa wakiwatangazia wamachinga hao kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia biashara huku wakitamka ya kwamba endapo wakikahidi watachukua bidhaa zao kwa nguvu na kuwachukulia hatua za kisheria. Hatahivyo,baada ya muda mfupi ndipo askari hao wali anza kutekeleza majukumu yao ya kusomba bidhaa hizo na kisha kuzipakia ndani ya gari lao huku wakivipeleka katika ofisi za manispaa ya Arusha. 

Hatua hiyo iliwapelekea wamachinga hao kujikusanya kwa pamoja na kisha kuvamia ghafla eneo la wazi wa Ermoil kwa kuvunja uzio wa mabati uliokuwepo na kisha kuanza kujigawia maeneo kwa kuyapima kwa kamba. Wamachinga hao zaidi ya 200 walivamia huku wengine wakitumia nafasi hiyo kupora mali mbalimbali zilizopo ndani ya eneo hilo kama mabati,nondo na saruji zilizokuwa ni mali za mtu anayedaiwa kumiliki eneo hilo. Katika heka heka za kugawana viwanja ndani ya eneo hilo wamchinga hao walikata miti iliyokuwemo ndani na kisha kuanza kuichoma kwa moto hali ambayo ilisababisha wingu zito la moshi kutanda hewani.

 Hatahivyo,wakati tafrani hiyo ikiendelea polisi waliokuwa wamesheheni kwenye magari yao walikuwa wakipita mara kwa mara kuzunguka eneo hilo lakini hawakuonekana wakifanya udhibiti wowote zaidi ya kuwaangalia wamachinga hao. Kitendo cha askari wa jeshi la polisi mkoni hapa kushindwa kuwadhibiti wamachinga hao kimetajwa kimetokana na uhaba wa askari kutokana na ugeni wa mkutano wa jana pamoja na kuhofia hali ya amani kuharibika jijini Arusha. 

Mkuu wa wilaya ya Arusha,John Mongella alilaani tukio hilo na kusema kwamba wamachinga hao wamevamia eneo hilo kimakosa kwa kuwa si la kwao huku akikitupia lawama chama kimoja cha siasa hapa nchini kwamba kimehusika katika kuhamasisha vurugu hizo. Alisema kwamba kwa sasa watakutana kujadili tukio hilo kwa undani kwa kuwa wana ugeni mkubwa lakini alisema kwamba kitendo cha wafuasi wa Chadema kupiga mawe gari la Cuf na mfuasi wake si cha kiungwana. 

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya jiji la Arusha,Omary Mkombole alisema kwamba kitendo cha wamachinga hao kuvamia eneo hilo ni kuvunja sheria na wataondolewa hapo hivi karibuni. Mkombole,mbali na kulaani tukio hilo alisema kwamba uongozi wa jiji umepanga maeneo mbalimbali ya kufanyia biashara na eneo hilo ni mali ya mtu binafsi ambapo alikuwa ameanza jitihada za kuliendeleza.

Mkutano wa Mbunge wa Mbeya Mjini(CHADEMA)Joseph Mbilinyi Igawilo, Mbeya

 Sehemu ya umati mkubwa wa wadau mbalimbali wa Chadema mkoani mbeya wakiwa kwenye mkutano wa hadhara
Mbunge wa mbeya mjini(CHADEMA)Joseph Mbilinyi aka Mr II -Sugu akiunguruma kwenye mkutano wa hadhara
  Sehemu ya umati mkubwa wa wadau mbalimbali wa Chadema mkoani mbeya wakiwa kwenye mkutano wa hadhara
Mbungwa mbeya mjini(CHADEMA)Joseph Mbilinyi aka Mr II -Sugu akisindikizwa na umati mkubwa wa wana chadema mkoani mbeya baada ya  kumaliza mkutani wake wa hadhara igawilo mkoani mbeya.Picha Zote na CHADEMA

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA AFRICAN GREEN REVOLUTION,ATETA NA MKE WA BILL GATES


 Rais Dk Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa 'African Green Revoultion' jijini Arusha leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa”African Green Revoultion mjni Arusha leo
 Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati alipokuwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa  Bill and Melinda Gates Foundation, Bi Melinda Gates wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 'African Green Revolution Forum 2012, uliofanyika jijini Arusha leo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa Alliance for a Green Revolution in Africa Dkt.Kofi Annan(kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Bill and Melinda Gates, Bibi Melinda Gates wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa” Africa Green Revolution Forum 2012,” uliofanyika katika ukumbi wa Ngurdoto mountain Lodge mjini Arusha leo.
 Baadhi ya  wajumbe na wageni waalikwa waliohudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 'African Green Revolution Forum 2012,' uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha leo.Picha na Freddy Maro-IKULU

Wednesday, September 26, 2012

Kutoka New York: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh Bernard Membe katika picha ya pamoja na Rais wa Marekani Barack Obama na Mkewe Michelle Obama

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe. Waziri Benard Membe, katika picha ya pamoja na Rais Obama na Mama Michele Obama wakati wa hafla ya Viongozi wa Nchi Wanachama za Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na Mhe. Rais Barack Obama jijini New York. Mhe. Waziri Membe yuko New York akiongoza ujumbe wa Tanzania akimuwakilisha Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

IKULU:RAIS JAKAYA KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MKURUGENZI MKUU WA KWANZA WA TAKUKURU, MEJA JENERALI (mstaafu) ANATOLI KAMAZIMA


 Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa  pole kwa mjane na ndugu wa wa Meja Jenerali Mstaafu  Anatoli Kamazima leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia  leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 utokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU.
Rais Kikwete akiongea na Brigedia Jenerali Mstaafu Tindamanyire, ndugu wa hayati Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima, leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es Salaam. Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu, Luteni Jenerali, Samwel Albert Ndomba. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 kutokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).Picha na IKULU
---
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Mkuu wa Majeshi  Jenerali Davis Mwamunyange kufuatia kifo cha Meja Jenerali Anatory Ruta Kamazima (Mstaafu) aliyefariki jana tarehe 25 Septemba, 2012 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Nimepokea kwa mshituko na huzuni nyingi habari za kifo cha Meja Jenerali Kamazima, ni pigo kubwa sana kwa Jeshi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Taifa kwa ujumla” Rais amesema katika salamu hizo.

Mchana wa leo Rais ameitembelea familia ya marehemu nyumbani kwao Tegeta kuwafariji wafiwa.

Marehemu alizaliwa mwaka 1946 katika kijiji cha Maruku, Mkoani Kagera. Alijiunga na Jeshi mwaka 1967, mara baada ya kuhitimu Chuo Kikuu mwaka 1966.

Marehemu Kamazima amesoma kozi mbalimbali za kijeshi hapa nchini na nchi za China, India, Uingereza na Misri na kulitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika ngazi mbalimbali ambapo mwaka 1989, aliteuliwa kuwa  Mkurugenzi wa Tume ya Kuzuia Rushwa Tanzania, hadi alipostaafu Juni 2003.

Rais amemuelezea marehemu Kamazima kama mzalendo na mtu aliyeipenda na kuitumikia nchi yake kwa weledi mkubwa, uaminifu na moyo mmoja.

“Nimemfahamu Marehemu kwa miaka yote ya utumishi wake jeshini na serikalini kama mzalendo, muaminifu na mwenye moyo wa kulinda nchi yake wakati wote” amesema “Marehemu Kamazima alikua mtu wa kutumainiwa sana katika nchi yetu na kamwe hatutamsahau kwa utumishi wake uliotukuka”.

“Tutamkumbuka na kumuenzi siku zote, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote na tunamuombea mapumziko mema Marehemu Kamazima. Amina”. Rais ameongeza.

Marehemu ameacha mjane, watoto na wajukuu.

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu.
DAR ES SALAAM