Wednesday, October 3, 2012

Taswira: Uzuri wa Jiji la Aleppo Syria Kabla ya vita. Sasa ni magofu tu yamebaki. Vita si mchezo.

Taswira: Milipuko minne iliyofuatana kwa dakika chache imetokea leo katika Jiji la Allepo Syris na kuuwa watu takriban 40.



http://www.islamicinvitationturkey.com/wp-content/uploads/2012/05/blast-in-Aleppo-.jpg
Takriban watu 40 wameuawa katika milipuko mitatu ya mabomu yaliyotegwa ndani ya magari katika mji wa Allepo nchini Syria
Mashambulio hayo yametokea katika eneo linalodhibitiwa na majeshi ya serikali. Mashambulio mawili yametokea katikati mwa mji na lingine nje ya ukumbi wa mji huo.
Picha za televisheni zimeonyesha uharibifu mkubwa huku majengo yakiharibiwa na pia barabara. Miili ya watu inabebwa kwa kutumia blanketi.
Mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi yameongezeka mjini Aleppo katika siku za hivi karibuni na kuugawa mji huo mara mbili.
Wapiganaji wa upinzani walianzisha upya mashambulizi wiki iliyopita katika jaribio la kunyakua maeneo zaidi ya mji huo.

AJALI YA MBALIZI MBEYA KIBAKA APEWA KICHAPO NAYE AFA









UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni huo ndio msemo pekee ambao naweza kuutumia katika kukujuza yaliyotokea mapema leo mchana katika ajali mbaya ya Mbalizi Mbeya Vijijini.
Wakati wengine wakiendelea kuokoa majeruhi wengine wamejikuta wakifanya tofauti na vile ilivyotegemewa pale kijana mmoja alipojitoa mhanga na kuingia katika mmojawapo wa waokoaji na kutaka kumchomolea fedha “ waswahili huita mshiko”.

Asalale kijana huyo ambaye hajafahamika jina mpaka mauti yanamkuta katika tukio hilo alikwidwa na mashuhuda wa ajali hiyo na kupewa kichapo cha mbwa mwizi wa kuku.

Wananchi wakichota mafuta kwenye ajali ya mbeya. Hatari tupu


KWELI BINADAMU TUNATOFAUTIANA 
HUKU TANKI LA MAFUTA LIKIENDELEA KUTEKETEA WENGINE WANAENDELEA KUKINGA MAFUTA HATARI TUPU

AJALI MBAYA ILIYOTOKEA ENEO LA MBALIZI MBEYA, MAGARI MAWILI YAGONGANA NA KUWAKA MOTO WATU KUMI WARIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWA ALIKUWEMO KATIKA AJALI HIYO NA KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO



 MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI
 WATU WAKIWA WAMEONGEZEKA KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA AJALI
  HAYA NI MABAKI YA GARI HILI AMBALO NALO LILIUNGUA LOTE
HIVI NDIVYO GARI HILI LILIVYO PINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI
 HII NI GARI NYENGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA
 HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
FIRE WAKIWA WAMEWAHI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO
 ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKA ENEO LA TUKIO AMBAPO MAGARI HAYO YAMESABABISHA VIFO VYA WATU KUMI.
MKUU WA MKOA WA MBEYA ALIYE VAA SUTI YA BLUE MH. ABASS KANDORO AKIWA ENEO LA AJALI.

Basi la Dar Express laungua Moto

Basi la  Dar Express limepata ajali ya kuungua moto leo asubuhi katika njia panda ya Dar, Arusha, Tanga (Segera) hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha. Katika ajali hiyo mizigo yote iliteketea kwa moto huo ambapo abiria wengi waliokuwamo kwenye gari hilo walikuwa ni wanafuzi.Picha na Samweli Mikuza