Thursday, September 13, 2012




Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)Mheshimiwa John Mnyika
---
Tarehe 9 Septemba 2012 baadhi ya vyombo vya habari viliandika habari kwamba wakazi zaidi ya 500 wa eneo la Ubungo Darajani karibu na Riverside wanalalamika kuishi kwenye mfereji wa maji taka wenye mafuta ya mitambo na mchanganyiko wa kemikali kadhaa zinazodaiwa kuzalishwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO).

Sijaridhika na majibu yaliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Felichism Mramba kwamba shirika hilo limedhibiti mfumo wa maji taka na haihusiki na tatizo hilo la kuchafua makazi na mazingira.
Kufuatia kauli hiyo, natoa wito kwa Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO kutoa majibu ya wazi kwa wananchi ni kampuni gani hasa inahusika na uchafuzi huo wa mazingira na kuchukua hatua zinazostahili kurekebisha mfumo uliopo.

Ikiwa hatua hazitachukuliwa nitaungana na wananchi kufikisha malalamiko yao kwenye mamlaka zinazohusika na usimamizi wa mazingira katika Manispaa ya Kinondoni na katika Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Waziri wa Nishati na Madini na Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO watoe majibu ya wazi kwa wananchi ni lini fidia ya wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi yanayozunguka mitambo ya kuzalishia umeme ya Ubungo itaanza kulipwa katika mwaka wa fedha 2012/2013 kutokana na kiasi cha shilingi bilioni 10 ambacho tayari kimeshaingizwa kwenye bajeti.

Izingatiwe  kwamba tarehe 04 Aprili 2012 nilifanya mkutano na wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga zaidi ya 500 katika kata ya Ubungo ambapo pamoja na mambo mengine nilitoa siku tatu kwa Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO kueleza hatua walizochukua katika kutekeleza ahadi waliyoniahidi  kwa nyakati mbalimbali kwenye mwaka wa fedha 2011/2012 wakati wa vikao vya kamati ya nishati na madini nilipohoji kuhusu hatma ya wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi jirani na mitambo ya umeme ikiwemo kuhusu uchafuzi wa mazingira unaoendelea.

Ikumbukwe kwamba mwaka 2004 baada ya mitambo kulipuka serikali iliahidi kuwalipa fidia wananchi husika na kuwahamisha, mwaka 2009 Serikali ikarudia tena ahadi hiyo lakini mpaka tarehe 4 Aprili 2012 ilikuwa haijatekelezwa hata kwa mtu mmoja.

Ndani ya siku hizo tatu, TANESCO ilitoa ahadi ya kuwa suala la fidia kwa wananchi litaingizwa katika bajeti ya serikali mapema iwezekanavyo na tayari kiasi cha shilingi bilioni 10 kimetengwa kwa ajili ya kuanza kulipa fidia ikiwa ni sehemu ya  Mradi wa Kuboresha Mifumo ya Umeme Katika Jiji la Dar es salaam (Kasma 3154).

Ili kuhakikisha kwamba mpango wa kulipa fidia ikiwa ni sehemu pia ya kuboresha mazingira ya eneo husika tarehe 27 Julai 2012 katika hotuba yangu bungeni kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani niliitaka Wizara ya Nishati na Madini ieleze iwapo kiasi cha 10,000,000,000 kilichotengwa kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi yanayozunguka mitambo ya kuzalishia umeme ya Ubungo kitatosha kukamilisha kazi hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili kuepusha uwezekano wa gharama kuongezeka kutokana na riba ya kuchelewa kufanya malipo kama ilivyotokea kwa miaka iliyopita.

John  Mnyika (Mb)
09 Septemba 2012

Je Malema ndiye Mugabe wa Afrika Kusini?



 
Wakosoaji wa Malema wanamuona kama mhemshaji. Wanasema kiongozi huyo wa zamani wa vijana analenga kutumia mauaji ya Marikana ambayo ndiyo mabaya zaidi kuwahi kufanywa na polisi tangu enzi ya ubaguzi wa rangi miaka 18 iliyopiya kuweza kujinufaisha kisiasa.

Malema anatumai kuwa chama tawala ANC, kitamuondoa rais Jacob Zuma kama kiongozi wake kwenye mkutano wa kitaifa wa chama hicho mwezi Disemba mwakani na hata kubatilisha uamuzi waliochukua wa kumfukuza kutoka kwa chama hicho.

Taarifa zinazohusiana

Tangu polisi kuwaua wachimba migodi 34 wa Marikana waliokuwa wanagoma tarehe kumi na sita mwezi jana, Bwana Malema amekuwa akizuru migodi ya Afrika Kusini akiwahutubia wachimba migodi, akiwashauri kutatiza kabisa shughuli katika migodi hiyo.
Mnamo Jumanne, aliitisha mgomo wa kitaifa na na kuwataka wachimba migozi kusitisha uzalishaji wa madini katika mojawapo ya migodi mikubwa ya dhahabu na madini ya platinum.
Kwa mujibu wa mdadisi wa maswala ya kisiasa William Gumede, Malema anatumia mauaji ya Marikana kujinufaisha kisiasa ili aonekane kama mkombozi wa waafrika weusi nchini humo ambao wamezongwa na umaskini. Lakini bwana huyu ana uungwaji mkono wa wafanyabiashara mashuhuri weusi.
Yeye hutembea bila hofu, katika maeneo ya vitongoji duni kabla ya kutoweka katika maeneo ya kifahari.
"ni vigumu kumfungia Malema njia zake. Yeye hutumia lugha safi ya kuwashawishi watu anaowalenga.''anasema bwana Gumede.
Gumede anamfananisha Malema na wanasiasa wa chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF, kinachoongozwa na rais Robert Mugabe.
"wao hutoa matamshi makali kuhusu maswala ya kijamii.Inapokuja kwa swala la uchumi , wao hutumia matamshi ya ujamaa wakati kimsingi wao ni mabepari ambao hutumia serikali kujibinafsisha maslahi yao,'' anasema Gumede.
'Hafai hata kwa demokrasia'
Tangu mauaji ya wafanyakazi wa mgodi wa Marikana unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin, ambayo ipo katika masoko ya hisa ya London na Johannesburg, Malema amepiga jeki, wito wake wa kutaka migodi kutaifishwa.
"waingiereza wanapata pesa nyingi sana kutoka kwa mgodi huu.Sio waingereza waliouawa. Ni ndugu zetu waafrika,'' alitoa matamshi hayo ambayo yanafanana na kauli ambayo hutolewa sana na chama cha Zanu-PF nchini Zimbabwe.
Pia alimfananisha afisaa mkuu mtendaji wa kampuni ya Lonmin Cyril Ramaphosa ambaye ana ushawishi mkubwa katika chama cha ANC, kama kikaragosi cha wazungu na wageni nchini humo.
Raia wengi wa Afrika Kusini wameonekana kughadhabishwa na serikali.
"kila mgodi una mwanasiasa ndani yake. Wao hupewa pesa kila mwezi, pesa wanazoziita hisa. Lakini ni malipo ya kutoa ulinzi kwa wazungu dhidi ya wafanyakazi weusi.'' Malema alidai
Bwana Gumede anasema matamshi kama hayo yanasikizwa sana na wananchi wengi maskini.
Kuhusu matamshi ya bwana Malema kwa mchimba migodi anayeishi katika vitongoji, ni ya kweli. Wakati akizungumzia uzalendo, wanapata matumaini ya kunufaika na utajiri wa madini nchini Afrika Kusini.
Malema anasemekana kutoa wito wa uzalengo kwa niaba ya wafanyabiashara katika jamii ya waafrika kusini weusi.
"wengi wa wafanyabiashara hao weusi walichukua mikopo kununua migodi kwa hivyo wana madeni chungu nzima. Ikiwa migodi itataifishwa itakuwa afueni kubwa kwao," anasema Gumede.
Malema pia ametumia mzozo huu kushinikiza wito wa kutaka rais Jacob Zuma ajiuzulu, akiwaongoza wachimba migodi, katika wito wao wa ''tumechoka na Zuma''.
'' Leo tunaishi maisha mabaya zaidi hata kuliko wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi. Tunauawa na watu wetu. Tunakandamizwa na serikali yetu,'' alisema Malema.
Lakini chama tawala kimemtaka Malema akome kutumia mauaji ya Marikana kujitafutia umaarufu.
Wadadisi wanasema kuwa Robert Mugabe huzua mchanganyiko wa maoni nchini Afrika Kusini. Wengi wanamuona kama mwenye kiburi na anayeamini kuwa utawala unapaswa kuwa wake peke yake.
Kitu muhimu kumhusu Malema ni kwamba, wakati kuna maandamano yanayohusu umaskini yeye huwa hakosekani pale. Kwa hivyo yeye hujaza penzo ambalo viongozi wamekosa kujaza. Na hivyo ndivyo anasalia kuwa vinywani mwa wengi.

SOURCE: http://www.bbc.co.uk/swahili  

Kero na ghadhabu katika nchi za Kiarabu



Kero na ghadhabu katika nchi za Kiarabu

Kumezuka ghasia zaidi nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo kati ya polisi na waandamanaji wanaokashifu filamu ambayo wanasema kuwa inakejeli imani ya Kiislamu.
Runinga ya Misri ilionyesha gari likiteketezwa moto na watu wengine wakikimbia vitoza machozi.

Taarifa zinazohusiana

Wakati huohuo maafisa wa Marekani wanasema serikali ya nchi hiyo inachunguza ikiwa mashambulio ya jumanne kwenye ubalozi wa Marekani katika mji wa Libya wa Benghazi yalikuwa ni ya kupangwa au la .
Balozi wa Marekani nchini Libya , Christopher Stevens, aliuawa .
Maafisa wa Marekani wameelezea mashambulio hayo kama yenye utata na yenye kupangwa kitaalamu na kuna tetesi kwamba makundi ya jihad huenda yalihusika .
Awali ilifikiriwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa na uhusiano na maandamano ya kupinga filamu iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed.
Takriban waandamanaji mia mbili wamekusanyika karibu na ubalozi wa Marekani mjini Cairo Misri kwa usiku wa pili kuelezea hasira yao juu ya filamu hiyo .

Aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya Christopher Stevens
Awali waandamanaji walirusha mawe kwenye ubalozi huo na vikosi vya usalama vikafyatua mabomu ya kutoa machozi kuwa tawanya.
Watu wenye silaha waliokuwa na maguruneti walichomo moto jengo la ubalozi na walioshuhudia wanasema watu hao walizingira eneo hilo.
Rais Obama amelaani vikali shambulio hilo na ameahidi kushirikiana na serikali ya Libya kuwafikisha mbele ya sheria wahusika
SOURCE: http://www.bbc.co.uk/swahili/habar

Kero na ghadhabu katika nchi za Kiarabu



Kero na ghadhabu katika nchi za Kiarabu

Kumezuka ghasia zaidi nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo kati ya polisi na waandamanaji wanaokashifu filamu ambayo wanasema kuwa inakejeli imani ya Kiislamu.
Runinga ya Misri ilionyesha gari likiteketezwa moto na watu wengine wakikimbia vitoza machozi.

Taarifa zinazohusiana

Wakati huohuo maafisa wa Marekani wanasema serikali ya nchi hiyo inachunguza ikiwa mashambulio ya jumanne kwenye ubalozi wa Marekani katika mji wa Libya wa Benghazi yalikuwa ni ya kupangwa au la .
Balozi wa Marekani nchini Libya , Christopher Stevens, aliuawa .
Maafisa wa Marekani wameelezea mashambulio hayo kama yenye utata na yenye kupangwa kitaalamu na kuna tetesi kwamba makundi ya jihad huenda yalihusika .
Awali ilifikiriwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa na uhusiano na maandamano ya kupinga filamu iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed.
Takriban waandamanaji mia mbili wamekusanyika karibu na ubalozi wa Marekani mjini Cairo Misri kwa usiku wa pili kuelezea hasira yao juu ya filamu hiyo .

Aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya Christopher Stevens
Awali waandamanaji walirusha mawe kwenye ubalozi huo na vikosi vya usalama vikafyatua mabomu ya kutoa machozi kuwa tawanya.
Watu wenye silaha waliokuwa na maguruneti walichomo moto jengo la ubalozi na walioshuhudia wanasema watu hao walizingira eneo hilo.
Rais Obama amelaani vikali shambulio hilo na ameahidi kushirikiana na serikali ya Libya kuwafikisha mbele ya sheria wahusika
SOURCE: http://www.bbc.co.uk/swahili/habar

'Innocence of Muslims' Trailer Part 7 [HD] - Egypt Protest Film

'Innocence of Muslims' Trailer Part 6 [HD] - Egypt Protest Film

'Innocence of Muslims' Trailer Part 6 [HD] - Egypt Protest Film

Kilichopelekea Balozi wa marekani Libya kuuwawa ni hiki ('Innocence of Muslims' Trailer Part 2 [HD] - Egypt Protest Film)

Wednesday, September 12, 2012

ONLY IN TANZANIA!


"ONLY IN TANZANIA!

   Yapo Maajabu mengi sana...Ila Maajabu Makuu Yaliyopo Tanzania ni Haya hapa;
     

 1. Mmoja wa Majaji Walioteuliwa kwa Mujibu wa Tundu Lissu Kumbe ndo
    kwanza anasoma shahada so darasani nae anasoma"What is Law of      Torts" then anapata SUP...U can Only find in TZ....afu mwalimu wake ni advocate inakuwaje akimpelekea kesi Jaji wa aina hiyo??

 2. Serikali Makini ambayo sio dhaifu ina Watumishi Hewa 9,949
    wanaopata Mshahara ambao Jumla ya hela inayopotea ni kama Bil 70
    ambazo zingetumika kulipa Madaktari na walimu, lakini Serikali
    inasema haina hela, hawana hela ya kulipa walimu na Madaktari ila
    wanazo za Watumishi hewa...Only u can find in TZ.

 3. Serikali Ya Uingereza Ilirudisha Chenji ya RADA, Serikali ikasema
    hela inapeleka Kununulia Vitabu kwa Ajili ya Shule Nchi nzima, Kumbe Kampuni iliyopewa tenda ya Kusambaza Vitabu nchi nzima ilitoa rushwa ya US$ 500,000 kupata tender Serikali ya Uingereza imeifungia miaka 7, You Can Only find in TZ.

4. Wanafunzi Waliofaulu Darasa la Saba get me well waliofaulu darasa
   la 7 kwenda Sekondary Hawajui Kusoma wala Kuandika, Je waliofeli
   Watakuwa hawajui kufanya nini??...You Can Only Find In Tanzania
  
  5. Washiriki wa Michezo ya Kimataifa (sijataja Mchezo wala
     mashindano) wako watano (5) lakini wanaowasindikiza Washiriki wako 12 You can Only find in Tanzania......

 6. Sehemu Pekee ambaye Mtu uliyetaka Kumdhuru kwa Kukusumbua then
    unaomba Umlinde (refer to Dr. Ulimboka's Case)..Yaani Mbwa Mwitu
    anaomba kazi ya Kulinda Mbuzi......You Can Only find in Tanzania..

  7.Only in Tanzania serekali inaweza kabisa kulipisha watu ushuru wa sticker ya fire Bila kuuliza kama una huo mtungi wa kuzimia moto wala kukagua gari wala kukupa hiyo sticker Na wananchi wake wakakubali na kunyamaza tu.

  8. Only in Tanzania hata rais hajui ni kwanini raia wake ni masikini?

       
Yapo Maajabu Mengi sana Lipi nimesahau???" Ongezea Moyoni
Source: http://just90.justhost.com/mailman/listinfo/members_nwb.or.tz