KATIBU Mkuu mstaafu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni Yusufu Makamba
---
KATIBU Mkuu mstaafu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni Yusufu Makamba, amesema Halmashauri
Kuu ya Taifa (NEC), ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) imefanya kazi nzuri kwa kuwa imesajiri supa timu ya kucheza ligi ya mwaka 2015.Makamba ametabiri kuwa kazi
nzuri iliyofanywa na NEC mjini Dodoma wiki iliyopita itakiwezesha chama
hicho kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge
mwaka 2015.
Kauli hiyo aliitoa jijini Dar
es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kuzindua kisima cha maji kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana Low
Church Parishi ya Ukonga Mazizini ambapo alialikwa kuwa mgeni rasmi.
“Nasema kama mwanachama wa CCM,
lakini pia kama Katibu Mkuu Mstaafu wa chama, tumesajiri wachezaji wa
super ligi ya mwaka 2015, wanaosemaCCM itakufa watakufa wao,”alitamba Makamba.
Aliongeza“Naamnini kuwa sisi
tumesajiri vizuri,maana usajili ni mzuri, kila aliyesajiliwa akipata
nafasi ya kushinda afanye yale yanayotakiwa”.Alisema katika uchaguzi
huo wao walizingatia zaidi kuunda timu itayochochea ushindi mwaka 2015
na si vinginevyo.
Wakati huo huo Makamba alihimiza
mshikamano miongoni mwa waamini wa kanisa hilo akionya kujiepusha na
majungu na fitina kwa kuwa sasa tabia hiyo mbaya imejikita mpaka
makanisani.
Alisema licha ya kuwepo maandiko
yanayowataka waumini kutii mamlaka lakini wapo watu wanayapiga teke
maandiko hayo na hivyo kuwadharau wapakwa mafuta wa Mungu hadi kufikia
hatua ya kumvua kofia wakiwa madhabahuni.
“Siku hizi majungu na fitina
vimeingia mpaka kanisani, maandiko yanasema kutii mamlaka lakini watu
wanamvua kofia hata askofu,”alisema Makamba.Makamba alialikwa katika
uzinduzi wa kisima hicho kilichogharimu zaidi ya sh. milioni 10 kutokana
kanisa hilo kuthamini mchango wake.
Katibu wa Kanisa hilo Keneth
Elia alisema Februari 26, mwaka huu Makamba alikuwa mgeni rasmi katika
harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa kisima
hicho.Alisema Makamba alichangia matanki mawili kila moja lina lenye
ujazo wa lita 5000 na mabomba yaliyosaidia kusambaza maji hayo.
No comments:
Post a Comment