Tuesday, October 2, 2012

Watu 36 wafa maji baadaa ya boti mbili kugongana huko Hong Kong








Hong Kong - Angalau watu 36 wamekufa na kadhaa wamejeruhiwa wakati kivuko kilichokuwa kibebeba watu 120 kugongana na feri nyingine kusini kwa kisiwa cha Hong Kong. Kivuko icho kilikuwa kimebeba wafanyakazi wa kampuni ya Hong Kong Electric.

Kivuko  hichi ni mali ya Kampuni ya Hongkong Electric, ambayo inamilikiwa na billionaire Li Ka-shing, ambapo alikuwa akichukuwa wafanyakazi wake na familia zao kwenda kuangalia fireworks katika mji wa Victoria kwa ajili ya kusherehekea siku ya Taifa ya china.
 
Waathirika walisema walikuwa na muda kidogo wa kuvaa majacket ya kuokoa maisha (life jackets) kwani maji yaliingia kwa kasi sana kwenye sehemu ya abiria. "Ndani ya dakika 10, meli ilikuwa imeshazama.  Sisi ilibidi kusubiri angalau dakika 20 kabla ya waliokolewa.," Alisema mmoja mwanaume aliyenusurika kwenye ajali hiyo.

Baadhi ya waathirika walivunja madirisha na kuogelea hadi pwani. "Tulidhani tulikuwa tunaenda kufa , kila mtu alikuwa amekwama ndani.," Alisema mwanamke wenye umri wa kati.

Huu ni mkasa mbaya zaidi kuikumba Hong kong tangu mwaka 1996 wakati zaidi ya watu 40 walikufa kwa kuteketea kwa moto uliozika katika jengo moja la kibiasharia.
Source: Reuters
 

No comments:

Post a Comment