Herny Kilewo
---
Mh.
Rais nitumie njia hii ya maandishi baada ya kutumia njia ya majukwaa
na matamko mbalimbali kuikosoa serikali yako na chama chako cha ccm..
Mh. Rais nimeamua kuandika baada ya leo kusikiliza mjadala mkali sana wa
Amani ya nchi yetu ambao ulikuwa unaendeshwa na kituo cha STAR TV leo
16/10/2010 Wazungumzaji wa mjadala huu walikuwa ni Mh. Tundu Lissu
Mkurugenzi wa chama changu wa sheria na haki za binadamu na Mbunge wa
Singida, Nape nauye katibu wako wa uenezi wa chama chako,pamoja na
muwakilishi kutoka chama kingine cha siasa.
Mh.Rais. baada ya mjadala huwo mkali ambao kama kawaida wa viongozi wa
chama Tawala kutumia fursa kama hizo kuhadaa umma, ukanipekea kukumbuka
utawala wa awamu ya tatu na awamu hii ya nne.
Mh.Rais. Kabla ya ujio wa Awamu ya Tatu ya uongozi wa serikali,watu
waliaminishwa kupitia ahadi za TANU (1962) haswa ahadi ile ya
Tano(UTUMISHI KWA UMMA NA UWAJIBIKAJI) wengi hatukuweza kujua madhara
yanayoweza kulikumba taifa kama ahadi(utumishi kwa umma NA HAKI YA
MWANANCHI) hii inakiukwa.
Mh.Rais. Katika awamu ya tatu,madhara yalijithihirisha wazi wazi kwa
uamuzi wa viongozi wa serikali ya chama cha mapinduzi(ccm) kuuziana
nyumba kwa bei ya kutupa na kukiuka sheria ambazo zilitungwa na serikali
hiyo hiyo kuhusu kanuni za uuzaji au ubinafisishaji wa mali na huduma
za serikali.Mh. Rais Hatua hiyo sikwamba ilikuwa inakiuka maadili ya
chama Tawala chenyewe yaliyomo katika ahadi hiyo ya Tano-chama amabacho
ndicho kinachozihodhi Ahadi hizo za Uraia Mwema, lakini Mh Rais. ni
uamuzi ambao umekiuka misingi ya utawala bora.
Mh Rais. kwa kuamua kuuziana mali za serikali bila kuzitangaza kufuatana
na kanuni za Zabuni ili kutoa nafasi kwa kila mwananchi kuo nyesha nia
yake ya kutaka kuzinunua mali hizo kwa bei anayoimudu, Mh Rais.
Serikali ilidhalilisha taifa letu kwa njia zifuatazo>
(a)Taifa lilinyimwa haki ya kupata mapato makubwa zaidi ambayo
yangeliwezesha Taifa kuwasaidia wananchi wengi zaidi kupata nyumba nzuri
za kisasa-jambo ambalo tunaelezwa kwamba ndilo hasa lilikuwa lengo la
zoezi hili. Mh Rais Tutalifikiaje lengo kwa kuliingizia taifa mapato
kidogo tu wakati amabapo tungeliweza kupata zaidi? Wahusika hao mpaka
sasa wamechukuliwa hatua gani juu ya kuliingizia taifa hasara?
(b)kwa kukiuka sheria zetu wenyewe za utangazaji wa zabuni tunapotaka
kuuza ama kubinafsisha mali za umma au kununua mali (RADA) Au huduma
ilikupata bei nzuri zaidi kwa kuchagua mzabuni amabaye angelinunua mali
zetu(NBC) kwa bei ya juu zaidi au anauza mali au huduma zake kwa bei ya
chini zaidi, Mh Rais. sielewi Amani ipi tunayoizungumzia ya Mtanzania
kuendelea kukaa kimya huku taifa likitafunwa,Amani hiyo ipo kwa
viongozi wa chache wanaoneemeka na mali za umma huku Mwananchi wa
kawaida akiishi kwa maisha ya Hofu kwakutokujua kesho yake, Mnatoa
polisi barabarani kwa wingi kuzuia maandamano ya amani ya CHADEMA na
mikutano ya hadhara huku mkishindwa kuweka vizuizi vya kutumia askari
kuweka mitengo kwa wala rushwa na kuwakamata,Mh.Rais.vibaka wanachomwa
kwa moto ama kupigwa na kuuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa ugumu
wa maisha, huku viongozi wanaoliibia taifa hili kwa kalamu wakiendelea
kuitwa mafisadi na kuendelea kuishi bila wasi wasi kana kwamba hamna
wa kuwawajibisha.mtawala mzuri anaheshimu sheria zake na kujali misingi
sahihi ya uendeshaji wa mambo ya taifa kama walivyokuwa Hayati mwalimu
Julius Nyerere,Hayati Abeid Amani Karume na Hayati Sokoine.
Tuige Mifano yao ambayo ililijengea Taifa hili heshima kubwa sana ndani na nje ya nchi kwa mfano
(i)1978 kulitokea vifo katika Gereza la shinyanga katika hali ya
kutatanisha,Hivyo serikali ilibidi iwajibike kwa tukio hilo maana
lilitokea mikononi Mwake na mahabusu wale walikuwa wamewekwa humo ndani
na serikali. Mh Rais. swali lilikuwa nani awajibike? Rais? Makamu wa
Kwanza wa Rais? Makamu wa pili wa Rais na Waziri mkuu au nani?
Mh Rais Kwa utaratibu mzuri anayewajibika ni yule kiongozi Mwenye
Dhamana inayohusiana na tukio hilo maana yeye ndiye aliyekabidhiwa ya
siku hadi siku ya kusimamia kazi za wizara au Idara yake kwa niaba ya
serikali.
Mh Rais.katika tukio hilo ilionekanika kwamba Wiazara Tatu ndizo
zilihusika, ya kwanza ilikuwa ni wizara ya mambo ya ndani ambayo
kiongozi wake alikuwa ni Mzee Alli Hassani Mwinyi. Lakini mshauri mkuu
mwingine wa Urais alikuwa ni Waziri aliyekuwa na Dhamana ya kusimamia
Usalama wa Taifa;ambaye kwa wakati huwo alikuwa ni Peter Siyovelwa.
Wizara ya Tatu ilikuwa ni wizara ya Tawala za Mikoa ambayo iliongozwa na
Peter Kisumo. Lakini Tukio lilitokea mkoa wa shinyanga ambako Mkuu wa
Mkoa alikuwa ni Marco Mabawa.
Mh Rais. kwa hiyo kwa heshima ya uongozi wa wakati ule, Rais aliona ni
haki kuwawajibisha mawaziri hawo watatu pamoja na mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, hivyo wote walilazimika kujiuzulu,na nchi ikawa na amani,
Hivyo ndivyo waungwana wote duniani wanavyofanya.
Mh.Rais katika awamu yako hii kumetokea mauaji mara kadha wa kadha
badala ya viongozi husika kuwajibika serikali imekuwa ikikimbilia
mahakamani huku waliyohusika na makosa hayo kuendelea kuwa madarakani
wakati vyombo husika vikifanya kazi yake, ni hivi majuzi tu tukio la
Mwandishi aliyekuwa mikononi mwa polisi na kufia mikononi mwa polisi
mpaka sasa hakuna mkuu yeyote wa polisi ama waziri ama mkuu wa moa
aliyewajibika katika sakata hilo, Utawala bora tunaowaimbia Watanzania
ni upi? sijaona kiongozi akiwajibika kwenye maisha ama kwenye haki ya
mtanzania kuishi bali nimesikia Mawaziri wakiwajibika kisiasa kupisha
upepo upite huku wakilitia taifa hasara. Umma wawatanzania tungependa
kujua amani hii ni ipi?
(c)Kwa Halmashauri kuu ya CCM Kuruhusu uamuzi huu unaokiuka ''AHADI YAKE
MUHIMU YA UADILIFU INAYOWAKATAZA VIONGOZI KUTUMIA VYEO VYAO KWA FAIDA
ZAO"kutekelezwa bila halimashauri kuu hiyo kuikemea serikali yake,
kunakiweka chama hicho katika MTIHANI MKUBWA WA IMANI,KAMA ILIVYOSASA
WANANCHI HAWANA IMANI NA CCM. Mh Rais uamuzi huu unawafanya watu
waaminifu,waadilifu,wasio na ubinafsi na wanaolitakia taifa lao mema
kwanini wakiamini chama hiki kuwaletea utawala bora? Ni dhahiri ya kweli
sasa yakuwa CCM ya kweli ilikuwepo kipindi cha Mwalimu nyerere.
Nahitimisha.
Mh Rais.jambo la kujiuliza ni kwanini tabia hii ya Rushwa imekithiri?
jibu la haraka haraka ni kwamba hii imetokana na uamuzi wa Halimashauri
kuu ya CCM mwaka 1991. ambao uliondoa miiko ya uongozi na kuwaruhusu
Viongozi wa kujilimbikizia mali kwa kupokea mishahara zaidi ya
mmoja,kufanya biashara wazi wazi bila miiko yeyote ile. Kiongozi
asipotosheka na anayeweka tamaa za binafsi mbele badala ya utumishi kwa
umma, anayo nafasi kubwa ya kuuza haki za wananchi na hata nchi yenyewe
kwa faida zake binafsi. Hivyo ndivyo inavyotokea leo, na ndiyo maana
watu wananunua uongozi.
Mh. Rais HAtutasita kuusema ukweli kwa hofu eti ya kuwakosoa watawala na
kuogopeswa kwa kifungo ama jambo lolote lile, Tutaendelea kuusema
ukweli kwa usiku na mchana mpaka siku ya mwisho ya maisha yetu kwakuwa
tunaamini mwenye kutenda haki ni mungu peke yake hapa duniani ni kanuni
tu za kuishi....
HAKI ITENDEKE KWA WOTE WANAOHUSIKA NA KASHIFA MBALIMBALI WATOKE KWENYE
MADARAKA KUPISHA SHERIA KUCHUKUA MKONDO WAKE, NENO AMANI LIWE AMANI
KWELI KWA WATANZANIA WOTE KUTOKUWA NA HOFU NA KESHO YAO.
Ahsante sana
HENRY KILEWO
KATIBU MKOA WA KINONDONI NA KANDA YA DSM
MJUMBE MKUTANO MKUU TAIFA(CHADEMA)
NEVER SAY NEVER M4C WE HAVE THE POWER,
16/10/2012.