Sep
16
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipokea Mwenge wa Uhuru
kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Sumbawanga leo.
Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Mathew Sedoyyeka akipokea Mwenge wa Uhuru
kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya tayari kwa
kuanza mbio zake katika wilaya hiyo ambapo baadae utaenda Wilaya ya
Kalambo na kumalizia katika Wilaya ya Nkasi.
Viongozi
wa Mbio za Mwenge kitaifa wakiwa na viongozi wa Wilaya ya Sumbawanga
wakikimbiza mwenge katika moja ya barabara za Manispaa hiyo ikiwa ni
kuunga Mkono na kukagua mradi wa Sumbawanga Ng'ara ambao lengo lake kuu
ni kudumisha usafi katika Mji wa Sumbawanga. Mradi huo umeasisiwa na
Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya na kuzinduliwa rasmi na Mhe.
Makamu wa Rais Mohammed Gharib Billal alipokuwa ziarani Mkoani Rukwa.
Kiongozi
wa mwenge kitaifa mwaka 2012 Kapteni Honest Ernest Mwanossa akiwa na
wenzake pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakifanya maandalizi ya
kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa.
Kiongozi
wa Mbio za mwenge kitaifa akiwa anazungumza na wananchi wa Mkoa wa
Rukwa. Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru lengo lake kubwa ni kuhamasisha
miradi ya maendeleo pamoja na kuubiri amani na mshikamano ambao ndio
nguzo kubwa ya mafanikio ya nchi ya Tanzania. Alisema wale wote
wanaoipiga vita Serikali iliyopo madarakani hawaitendei haki kwani
maendeleo yote yaliyoletwa nayo ikiwemo barabara na mashule wanazitumia
wote bila kujali dini zao au vyma vyao.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwapa utaratibu wa
waendesha Pikipiki (Bodaboda) namna ya kupokea Mwenge wa Uhuru. Jumla
ya waendesha Pikipiki 100 walishirikishwa katika mapokezi ya Mwenge huo
wa Uhuru.
Baadhi
ya viongozi wa Mkoa wa Rukwa kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Sumbawanga Methew Sedoyyeka, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Samson
Mashalla, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi na RPC wakishuhudia mapokezi hayo.
Kiongozi
wa mwenge kitaifa mwaka 2012 Kapteni Honest Ernest Mwanossa
akipandikiza Samaki katika bwawa la kufugia Samaki lililopo Mishamo
katika Manispaa ya Sumbawanga alipofika kukagua ufugaji wa samaki.
Nyuma yake ni waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kutafuta
taswira mwanana kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa wananchi.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiwasalimu wananchi wa
Mkoa wa Rukwa waliojitokeza katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga kwa
ajili ya kuupokea mwenge wa uhuru ambao umemaliza mbio zake Mkoani
Kigoma na kuwasili Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufanya mbio zake katika
Wilaya tatu za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi kwa muda wa siku nne.
Kwenye baadhi ya uzinduzi wa miradi baadhi ya wananchi walilazimika kupanda juu ya miti ili kuona matukio yote bila chenga.
Vikundi vya ngoma vilikuwepo kutoa burudani.Picha na Habari na Hamza Temba-Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Subscribe to:
Posts (Atom)
No comments:
Post a Comment