John Heche , Septemba 17, 2012 alifungua Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha kilichohudhuriwa na wajumbe kadhaa kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.Kikao hicho kilipanga kujadili ajenda mbalimbali za Vijana na baadaye kufikia kutoa tamko la pampoja kuhusiana na masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.Hata hivyo katika Kikao hicho , Bavicha kupitia Mwenyekiti wake wa Taifa , walimkaribisha Mwandishi wa Habari na Mtangazani wa zamani wa TBC, Jerry Muro ili aweze kuwasalimia wa wajumbe wa Baraza hilo walioanza kukutana tangu Septamba 14 hadi 18, mwaka huu.Katika salaamu zake , Muro alisema, yenye ni mwanaharakati na mtu anayependa kusema ukweli, hivyo kwake mtu kama huyo ni lazima amuunge mkono kama ilivyo kwa vijana wa Bavicha wanavyosimamia kusema ukweli na kuamua kuwaunga mkono kwa hilo.
Picha na Habari na John Nditi Mwenyekiti wa Bavicha Taifa
No comments:
Post a Comment