Wednesday, September 19, 2012

UNENE WA KUPINDUKIA UTAMWOKOA RONALD POST NA SINDANO YA SUMU?


 Post
 Kitanda cha kufania mauaji
 
 Mfungwa mwenye kitambi
 Waandishi wa habari wakikagua chumba ckabla mfungwa hajaletwa
 
 Mfungwa akiandaliwa tayari kwa kuuwawa

 
 dawa ya sumu ikiwa tayari (lethal injection)

 
 Muuaji (executioner) akiweka sumu katika mwili wa mfungwa

  Vifaa vinavyotumika
 
 
Ndugu Wakiomba Mungu Muujiza utokee ili ndugu yao asiuwawe
 Ndugu wakichukua maiti wao baada ya kuuwawa

Wanasheria wa mahabusu  mwenye uzito wa paundi 480 anayesubiri kuuwawa kwa kudungwa sindano ya sumu katika gereza moja huko Ohiyo marekani katika wamesema kwamba  mteja wao ana uzito mkubwa sana na isingefaa kuuwawa.
"Hakika, kutokana na hali yake ya kipekee kimwili na matibabu kuna hatari kubwa kwamba jaribio lolote la kutaka kumuua sasa litamfanya apatwe na maumivu makali ya kimwili na kisaikolojia. Ronald Post, mwenye miaka  53, ambaye alikuwa na hatia ya kumpiga  risasi hadi kufa karani wa hotelini Helen Vantz miaka 29 iliyopita.

Post, ambaye anatakiwa auwawe kwa sindano ya sumu (lethal injection) Januari 16, 2013, anasema kwamba mauaji yake yatakukutana matatizo kadhaa, ikiwa ni pamoja na ugumu wa kupata kwa urahisi mshipa wa damu kwa ajili ya sindano ya mshipa na uwezekano kwamba kwa uzito wake kawaida angeweza kuvunja taratibu zinazotumika  katika mchakato wa kumuuwa.

Katika sheria za magereza ya  Ohio mfumo wa kutekeleza adhabu ya kifo hutegemea sindano ya sumu

Jimbo la Ohiyo linatajwa kuwa la kwanza kuwa na watu wenye vitambi zaidi Marekani wakifuatiwa na Kansas. Asilimia 29.6 ya wakazi wa Ohiyo wanaelezwa kuwa na uzito wa kupindukia.
Msemaji wa Post Bw Joseph Wilhelm amekiri kuongezwa manjonjo juu ya afya ya Bw Post na kuendelea kusema kwamba maisha yake ni zaidi ya unene wake hivyo kutokumuua kwa sindano ya sumu kungekuwa na maana zaidi.

Vyombo vya habari vya Ohiyo vimeripoti kwamba, hii ni kesi ya kwanza kwa mtuhumiwa kukwepa kifo kwa sababu za unene.

Mwaka 1994, shirikisho jopo la mahakimu katika Jimbo la Washington lilitoa uamuzi kuwa Mitchell Rupe  aliyekuwa na uzito wa paund 400 alikuwa mzito  mno kwa kunyongwa na badala yake  alihukumiwa kifungo cha maisha jela. Hata hivyo, Rupe Alifia Jela mwaka 1986

Hata hivyo, mahabusu wengine waliojaribu kutumia kigezo cha uziko ili kukata rufaa hawakufanikiwa, kama vile katika kesi ya Richard Cooey  mwaka  2008 na Christopher Newton mwaka 2007. Hata hivyo, wafungwa hawa walikuwa uzito wa paund 200 pungufu ya Post.

Newton, ambaye alikuwa  wa Ohio, kuuwawa kwake kulichelewa kwa saa mbili kwakati wafanyakazi wa gereza wakifanya jitihada za kupata  mshipa kwa ajili ya kuingizia sindano ya sumu.

Marekani  ni kati ya nchi  20  duniani kati ya nchi 198 zilizoidhinisha rasmi adhabu ya kifo, kulingana na Amnesty International. Mwaka 2011 Marekani ilinyonga afungwa 43 na kati ya hao watano ni wa jimbo la Ohio.
China ndiyo nchi inayoongoza kwa kwa kutoa hukumu ya kifo zaidi duniani ingawa idadi kamili haijulikani.  Miongoni mwa mataifa ambayo taarifa ya idadi yao ya kunyongwa, Iran inaongoza orodha, na kwa uchache watu 360 waliuwawa mwaka 2011
Taarifa hii imetafsiriwa na Bahati Fortunato.

No comments:

Post a Comment