Monday, September 17, 2012

VURUGU ZANZIBAR

Kumekuwa na vurugu za hapa na pale, Polisi kupambana na vijana kwenye kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi mdogo kumchagua Mwakilishi wa jimbo la Bububu Zanzibar jana. 
   Polisi wa kuzuia ghasai wakijaribu kuwadhibiti baadhi ya vijana waiokuwa karibu na kituo cha upigaji kura
   Polisi wa kutuliza ghasia wakiwa katika doria eneo la Bububu
  Askari za Kutuliza Ghasia (FFU) akiwa amemweka chini ya ulinzi kijana mmoja wakati wa zoezi ya kuhesbu kura katika jimbo la Bububu
 Kijana akitumbukiza kura yake kwenye kisanduku cha kupigia kura jwenye kituo cha Shule ya Bububu Zanzibar
 Kiongozi wa chama cha siasa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha kupigia kura jana.
   Mawakala wa vyama tofauti vilivyoshiriki katika uchaguzi wa bububu wakifuatilia kwa makini maendeleo ya zoezi hilo
Kumekuwa na vurugu za hapa na pale, Polisi kupambana na vijana kwenye kituo cha kupigia kura wakati wa  uchaguzi mdogo kumchagua Mwakilishi wa jimbo la Bububu Zanzibar jana. (pichani) Polisi wa kuzuia ghasia wakisaidiwa na kikosi cha Valantia  kuwaondoa vijana   waliojikusanya karibu na kituo cha kupigia kura  kwenye  Shule ya Bububu. Picha zote na Martin Kabemba.
--
Chama cha Mapinduzi kimeshinda katika Uchaguzi Mdogo uliofanyika leo katika Jimbo la Bububu kutokana na kifo cha aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Salim Amour Mtondoo.

Akitangaza matokeo Misimaamizi wa Uchaguzi huo Suluhu Ali Rashid amesema kuwa Hussein Ibrahim Makungu wa CCM ameshinda kwa kupata kura 3371 sawa sawa na asilimia 50.7ambapo Issa Khamis Issa wa CUF amepata kura 3204 sawa sawa na asilimia 48.2

Aidha Suluhu amesema kuwa Mgombea wa Chama cha ADC Zuhura Bakari Mohamed amepata kura 45 sawa sawa na asilimia 0.7 wakati Abubakar Hamad Said wa Chama cha AFP amepata kura 8 sawa sawa na asilimia 0.1, Mtumweni Jabir Seif wa Jahazi Asilia amepata kura 7 sawa sawa na asilimia 0.1,Haroun Abdulla Said wa NCCR amepata kura 3 sawa sawa na asilimia 0.0, Suleiman M.Abdulla wa NRA amepata kura 1 sawa sawa na asilimia 0.0 Seif Salim Seif amepata kura tatu sawa sawa na asilimia 0.0 na Juma Metu Domo wa Chama cha SAU amepata kura 4 sawa sawa na asilimia 0.1.

Jumla ya kura 6720 zilipigwa sawa sawa na asilimia 68.6.Kura 74 ziliharibika sawa sawa na asilimia 1.1Kura halali ziliozopigwa zilikuwa 6646 sawa sawa na asilimia 98.9na waliojiandikisha walikuwa 9799.

IMETOLEWA NA 
IDARA YA HABARI 
MAELEZO ZANZIBAR16/9/2012

No comments:

Post a Comment