Monday, September 17, 2012

Mwakiembe Ujerumani

  Mhe. Waziri wa uchukuzi Dk Mwakyembe katikati akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Ahmada R. Ngemera (kushoto) na Afisa wa Wizara ya mambo ya Nje, Ali Ubwa Mussa (Kulia).
   Mhe Waziri wa mawaziliano Dk Mwakyembe akikagua moja ya ndege zilizokuwepo katika maonesho
  Mhe. Waziri, Dk Mwakyembe akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa ndege za Airbus, nchini Ujerumani (hayupo pichani) pembeni yake ni Mhe. Balozi wa Tanzania Ujerumani..
   Mhe. Waziri  Dk Mwakyembe akiongoza ujumbe wa Tanzania  katika Majadiliano na Uongozi wa Sekta ya Usafiri wa Anga, Germany.
  Mhe. Waziri na ujumbe wake wapo Berlin kuanzia tarehe 15 hadi 19 sept, 2012. Moja ya tukio muhimu ni kusainiwa Mkataba wa Ushirikiano wa Usafiri wa Anga (Bilateral Air Services Agreement - BASA) baina ya nchi hizi mbili tarehe 17 Sept. 
--
Aidha, jana tarehe 16 sept, Mhe. Waziri na ujumbe wake walitembelea maonyesho ya Kimaitaifa ya sekta ya Usafiri wa Anga yaliofanyika hapa Berlin. Aidha kwa nyakati mbalimbali, Mhe. na ujumbe wake watakutana na wafanyabiasha na wawekezaji mbalimbali hususani katika sekta ya usafiri (Anga, reli na meli).

Baada ya ziara ya hapa Ujerumani, ujumbe wa wataalam (tu) aliofuatana nao Mhe. Waziri utaelekea the Hague Uholanzi kwa ajili ya majadiliano mengine kuhusu usafiri wa anga tarehe 19 hadi 21 sept. .

No comments:

Post a Comment