Tuesday, September 18, 2012

Mahakama yabana picha za Kate Middleton







Kate na mumewe William
Mahakama nchini Ufaransa, imetoa amri ya kusitisha kuchapishwa tena, kuuzwa au kusambazwa kwa picha za mke wa mwanamfalme wa Uingereza, Kate Middleton akiwa nusu uchi.
Wendesha mashtaka wangali kuthibitisha ikiwa kuna misingi ya kufungua kesi ya jinai dhidi ya mpiga picha aliyepiga picha hizo za Kate na mumewe William wakiwa katika likizo ya faragha nchini Ufaransa.
Amri ya mahakama imekuja baada ya wanandoa hao wawili kuchukua hatua za kisheria dhidi ya jarida la udaku la
(Closer) nchini Ufaransa kwa kuchapisha picha hizo pamoja na kuzisambaza.
Waliochapisha picha hizo wamepewa siku moja na mahakama kuzikabidihi kwa Kate na mumewe picha zenyewe.
Jarida hilo litaweza kufainiwa dola elfu nane ikiwa litakiuka amri ya mahakama, kuzichapisha na kuzisambaza picha hizo.
Wawili hao wanasema kuwa jarida hilo liliingilia maisha yao ya faragha kwa kuchapisha picha hizo.
Uamuzi wa mahakama umejiri baada ya viongozi wa mashtaka kusema kuwa walikuwa wanataka kufahamu ikiwa wangeweza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya jarida hilo.

No comments:

Post a Comment