Monday, September 17, 2012

Serengeti Fiesta Morogoro Funika Bovu

 Michael Jackson wa Morogoro akionesha umahiri wake kuchenza nyimbo za The Wacko Jacko.
Msanii chipukizi kutoka nyumba ya vipaji,THT,Alini Nipishe akiimba na shabiki wake jukwaani usiku huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea.
 Mmoja wa sanii chipukizi katika shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Ney Lee akionesha kipaji chake cha kuimba jukwaani usikuwa kuamkia leo
Msanii muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Recho akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro,ambapo wakazi kibao wa mji huo (hawapo pichani) wamejitokeza kwa wingi.
 Mkali wa Supa Nyota,Jo Meka akikamua jukwaani.
Mmoja wa wasanii chipukizi kutoka mjini Morogoro akiimba jukwaani.
Morogoro kuna vijana wengi wenye vipaji,ambao kiukweli wameonesha vilivyo kwenye jukwaa la Fiesta 2012 usiku huu.
Msanii mahiri katika mahadhi ya Mduara AT akiduarika na mmoja wa densa wake jukwaani usikuwa kuamkia leo
 Msanii mwingine mahiri katika fani ya filamu Ray Kigosi akicheza sebene mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa Morogoro  na vitongoji vyake waliojitokeza usiku huu kuwashuhudia wasanii mbalimbali wakitumbuiza kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012.
 Msanii nyota wa Filamu hapa nchini Wema Sepetu akiwaonjesha washabiki wake kipaji kingine mbadala ya uigizaji usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012
 Baadhi ya wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiwashukuru wakazi wa Morogoro kwa namna moja ama nyingine na kuwakubali vilivyo katika fani ya uigizaji.
  Bonge la bwana a.k.a Dj Ben a.k.a JB akimtunza hela msanii wa kundi la Ze Comedy Orijino,Mpoki,kulia kwake ni Ray Kigosi akiwahamasisha mashabiki wapige mayowe na makofi
Pichani juu na chini ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dayna na kundi lake la Wakali wa Classic wakitumbuiza jukwaani
Pichani kulai ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro,Mh Joel Bendera akisoma mshindi wa Piki piki zinazotolewa na kampuni ya Push Mobile katika mchakato mzima wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,kati ni Meneja masoko wa kampuni ya Push Mobile, Rodney Lugambwa pamoja na msanii wa kundi la Ze Comedy,Mpoki akifuatilia kwa makini tukio hilo.
 Pichani kulia ni Ofisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh Joel Bendera ambaye ni mgeni rasmi usiku huu ndani ya uwanja wa Jamhuri,wakati tamasha la Serengeti likiendelea kufanyika.
 Mkali wa kusugua mangoma,Dj Zero akifanya makamuzi yake.
 Wadau mbalimbali wa tamasha la Fiesta wakifuatilia burudani mbalimbali zikiendelea hivi sasa jukwaani.
 Wadau wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri usiku huu.
Ni burrudani tu ndani ya muonekano mpya wa tamasha la serengeti fiesta 2012.

No comments:

Post a Comment