Rais
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni
Jenerali Samuel Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo
jijini Dar es salaam. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa
wazi na Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini
kwa Umri.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael
Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo
Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) na maofisa
wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ (wa tatu
kutoka kushoto) na Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga mkuu wa JKT
walioapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Maofisa wa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto)
akimweleza jambo Rais Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) katika viwanja vya
Ikulu jijini Dar es salaam.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Saidi Meck Sadiki (katikati).
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel
Albert Ndomba akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Maofisa Waandamizi Wanawake wa
JWTZ. Kushoto ni Meja Jenerali Lilian Kingazi na Meja Jenerali Grace
Mwakipunda (kulia).
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia)
akiwaeleza jambo viongozi wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali
Saidi Mwema (wa pili kulia) na Kamishina wa Oparesheni wa Jeshi la
Polisi, Paul Chagonja . Kulia ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Devis
Mwamunyange.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
No comments:
Post a Comment